Linex ndiye msanii aliyetakiwa kuimba chorus ya ‘Salaam Zao’ ya Nay wa Mitego lakini




Nay Wa Mitego ameendelea kuwa kati ya wasanii ambao pindi watoapo nyimbo ni lazima zizue mijadala kutokana na aina yake ya uandishi wenye utata. Baada ya kutoa single yake mpya ‘Salaam Zao’ wiki iliyopita tayari mambo kadhaa yameshaanza kujitokeza.



Linex

Linex Sunday ndiye msanii aliyetakiwa kuimba kiitikio (chorus) katika ‘Salaam Zao’ ya Nay wa Mitego lakini kwa mujibu wake, kutokana na uzito na utata ulioko kwenye mashahiri ya wimbo huo unaowalenga watu mbalimbali kwa kuwataja majina alisita na kuahirisha kushiriki na baadaye nafasi yake kuchukuliwa na Neyba aliyeimba chorus.


Nay wa Mitego

Kupitia ukurasa wake wa Facebook Linex ameandika:
“Wimbo mpya wa ney wa mitego salaam zao mi ndo nilitakiwa kufanya chouras but sikufanya coz mashairi yake yalikua mazito na yananidiss had mm so nikaona niiache ipite salaam zinipate kigoma all stars haijafa but wahusika kila mtu yuko busy na maambo yake tunahitaji time kufanya somthn big tena#teamkimugina”.


Walter Chilambo

Msanii mwingine ambaye amepewa ‘salaam’ katika wimbo huo ni mshindi wa EBSS mwaka jana Walter Chilambo, ambaye jana (August 12) kupitia XXL ya Clouds Fm alijibu salaam za Nay kupitia wimbo huo.

Walter alithibitisha kupewa zawadi yake ya Million hamsini na waandaaji wa EBSS na kusema hawezi kuishi kama watu wanavyotaka sababu anamipango yake binafsi ya jinsi ya kuitumia pesa hiyo, hivyo hajui ni sababu zipi Nay wa Mitego amesema kitu ambacho hana uhakika nacho huku hawana hata urafiki wa kawaida.

Sehemu iliyomzungumzia Walter katika wimbo huo inasema “Hizi salaam ziende kwa mada Ritha na Bongo Star Search mshindi analipwa nini mbona kama magumashi, namuona Walter Chilambo kapigika ka zamani, Haji Ramadhani kachoka yuko kitaani Million 50 zao anazila nani acheni ubabaishaji wekeni mambo hadharani”…

Pia katika outro ya wimbo huo Nay anasema “Aah Walter Chilambo niaje mwanangu najua una hali mbaya kiuchumi Millioni 50 huna hata baiskeli, huna wewe hizmfikishie salaam madam Ritha mwambie sina tatizo naye”.

Nani mwingine aliyetumiwa salaam na Nay atajibu salaam hizo? Tusubiri.
Previous Post Next Post

Popular Items