Babu Tale ajibu tuhuma zilizozotolewa mwezi April kuwa kampuni yao ‘OSATA’ inaua muziki wa Tanzania




Meneja wa Tip Top Connection, Babu Tale jana alikuwa mgeni kwenye show ya Mkasi inayooneshwa kupitia kituo cha runinga cha EATV. Kwenye kipindi hicho, Tale alifunguka masuala mengi kuanzia alikoanza shughuli za umeneja na mambo mengine.

Jimmy Kabwe na Babutale kwenye KTMA
Kupitia Mkasi, Babutale alijibu email iliyosambaa mwezi April mwaka huu kuwa kuna kundi la watu watatu liitwalo OSATA linalomjuisha yeye, Said Fella na Suka ambalo linadaiwa kuia Bongo Flava na kuitwa Mafisadi wa Muziki.



“Mimi alinifuata Diamond wakati ametoka kugombana na Papaa, ‘Tale nataka unisimamie’. Nikasema nikimsimamia huyu peke yangu, halafu mimi nipo Tip Top Connection itanipa tabu. Mimi nikamfuata Fela tuwe tunafikisha muziki kwenye media house. Lakini mimi nina Diamond ambaye amenifuata tumsimamie lakini tusiwe tunamsimamia, anatulipa pesa yeye anakwenda na maisha yake. Wakati tunaongea maneno hayo Suka alikuwa karibu. Kwamba tufanye kitu kwa pamoja, Suka, Fella na Tale, tusaidie kufikisha ngoma kwenye media house. Tukafanya na Diamond, Sumalee akasikia, tukafanya na Sumalee, Ferooz akasikia, tukafanya na Ferooz, AY akasikia, tukafanya na AY wimbo aliofanya na Romeo, FA akasikia, tukafanya na FA Yalaiti. Kila mtu anayekuja kwetu anasema sitaki kwenda redioni kupeleka nyimbo,” alisema.

DSC_1452

Tale amesema kuwa hadi leo Osata inaendelea kumsimamia Diamond.
“Kila kitu kikubwa anachofanya Diamond, nathubutu kusema kwamba Tale yupo, Fela yupo. Tunauaje muziki kama hata namba moja sisi tunamsaidia katika kumsukuma? Huyo mtu aliyeandika hiyo email lakini anatujua kwenye upande wa mabaya tu.”
Katika hatua nyingine, Tale alidai kuwa yeye ndio meneja wa muziki Tanzania mwenye nyumba ya kifahari zaidi.
Alisema nyumba yake ambayo ipo Mbezi jijini Dar es Salaam ni ya kifahari kiasi ambacho akiiangalia hata yeye hushindwa kuamini kama ameweza kuijenga mwenyewe. Amesema anatarajia kuhamia kwenye nyumba hiyo ambayo tayari imekamilika baada ya mke wake kujifungua.

News via: bongo5
Previous Post Next Post