Kama Zamani Ya MwanaFa sasa inapatikana kwenye App ya Shazam



Screen Shot 2013-08-15 at 2.12.44 AM

Track ya MwanaFa ft kilimanjaro Band ni moja ya Track iliyobeba uzito baada ya kushirikishwa kundi la Mziki la wana njenje vijana wazee ambao wanaheshimika kwa kuwa kwenye maisha ya mziki kwa kipindi kirefu.
Track hii ambayo inapatikana kwenye mitandao maarufu duniani itunes na Amazon sasa imeongezeka kwa kupatikana kwenye application ya Shazam.
Shazam ni Application maarufu duniani ambayo inatumika kukufahamisha kupitia Smartphone yako kuwa ni nyimbo gani unasikiliza na inakupatia jibu la nyimbo hiyo na kukupa option ya kuinunua kama ulikuwa hujui jina la wimbo unaosikia kwa wakati huo.
Mara nyingi tumezoea kukuta kwenye application ya Shazam ni Track za ulaya ndio zimekuwa zikipatikana kwenye application hii.



Previous Post Next Post