Google imetangaza ofa kwa wanawake walio katika fani za computer science, computer engineering kutoka Afrika, Ulaya na Mashariki ya Kati kuhudhuria mikutano ya teknolojia itakayofanyika baadae mwaka huu.
Kampuni hiyo ya Google imesema ili kuhamasisha wanawake wengi kuhudhuria mikutano hiyo ya teknolojia na sayansi itatoa ruzuku ya mpaka EUR 1000 kwa wanawake watakaohudhuria ikiwa ni sehemu ya mpango wa kampuni hiyo unaoendelea wa kuwahamasisha wanawake kujiingiza zaidi katika maswala ya kompyuta na teknolojia.
Ili mwombaji aweze kupata ofa hiyo ya Google ni lazima awe mwanamke anayefanya kazi au kusoma Computer Science, Computer Engineering, au fani yoyote ya ufundi inayoshabihiana na mada ya mkutano. Sifa nyingine awe na historia nzuri ya kitaaluma pamoja na uwezo katika uongozi.
Waombaji wote watajulishwa matokeo ya maombi yao kwa barua pepe, takriban wiki 3-4 kabla ya tukio, na kwa wale watakaochaguliwa watapata maelezo ya ziada juu ya jinsi ya kujiandikisha kwa ajili ya mkutano na jinsi ya kupokea ruzuku ya usafiri wako.
Mikutano hiyo itafanyika Berlin, Ujerumani (September), Minneapolis, Marekani (October), Malta (September) pamoja na London, Uingereza (November).
Ingia hapa kusoma maelezo zaidi ya jinsi ya kutuma maombi.
Tags:
Technology