Duniani Kuna Mambo: Mfalme wa Saudi agharamikia matibabu ya Khalid Mohsin Shaeri, mtu mnene zaidi duniani, ana kilo 610




Mfalme wa Saudi Arabia, Abdullah amelazimika kugharamikia matibabu ya Khalid Mohsin Shaeri, mtu mnene zaidi duniani, mwenye kilo 610 ili kumrudisha katika hali ya kawaida.













Kutokana na unene, ukubwa na uzito wake, Khalid hawezi kutembea wala kusogea mwenyewe bila msaada wa kifaa maalum cha kuongea na kumbeba akiwa katika kitanda chake. Khalid ana umri wa miaka kati ya 18 na 20.
gordo-1_560x280


Khalid akinyanyuliwa juu kwa kifaa maalum
Mfalme Abdullah amelipia ndege maalum kumchukua Khalid Mohsin Shaeri iliyomchukua kumpeleka hospitali.
Kijana huyo hakuwahi kuondoka chumbani mwake kwa kipindi cha miaka miwili na nusu. Sehemu ya nyumba yao imevunjwa ili kuweza kumshusha kutoka ghorofa ya pili kilipokuwa chumba chake.
Mfalme aliaigiza Shaeri atibiwe miezi sita iliyopita lakini matibabu yalichelewa hadi pale kitanda maalum kingetengenezwa nchni Marekani.
Wizara ya afya ya Saudi Arabia imeshirikiana na jeshi la wananchi na Red Cross ili kumtoa ndani mgonjwa huyo.
Kutokana na rekodi za Guinness, Manuel Uribe kutoka Mexico ndiye aliyekuwa akishikilia rekodi ya mtu mzito na mnene zaidi duniani ambapo alikuwa na uzito wa kilo 560. Baada ya kuonekana na kuingizwa katika matibabu, kwa sasa amepungua na kufikia uzito wa kilo 444.
Source: CNN na Daily Mail
Previous Post Next Post

Popular Items