Feza na Nando ni wawakilishi wenye ushawishi mkubwa kwenye historia ya BBA, Tanzania







Alikuwepo Mwisho Mwampamba aliyekamata nafasi ya pili kwenye msimu wa kwanza wa Big Brother Africa na kurejea tena kwenye msimu wa tano wa Allstars.
mwsho
Mwisho Mwampamba
Akaja Richard Dyle Bezuidenhout aliyeibuka mshindi kwenye Big Brother Africa msimu wa 2.
richard
Richard
Alifuata Latoya kwenye msimu 3 mwaka 2008, ambaye hata hivyo akawa mshiriki wa kwanza kutoka.
latoya-tanzania-bba3-hm11
Latoya BBA 3
Baadaye alikuja Elizabeth Gupta kwenye msimu wa nne mwaka 2009.
kevin pam & family mackielycious.com
Elizabeth akiwa na mumewe Kelvin na mtoto wao
Big Brother Africa: Amplified akaenda Bhoke na Lotus.
bhoke-lotus-1
Bhoke na Lotus
Na kisha mwaka jana kwenye Big Brother Africa Stargame akaenda Hilda na Julio.
hj
Julio na Hilda
Mwaka huu kwenye BBA The Chase wameenda Ammy Nando na Feza Kessy.
ChaseFeza1LRG..............
Huenda kwasababu Ammy Nando na Feza Kessy wameenda katika kipindi ambacho watu wengi wapo kwenye mitandao ya kijamii kiasi cha kuona kwa urahisi namna walivyo na ushawishi lakini ni ukweli usiopingika kuwa wametoka kuwa na mvuto mkubwa si Tanzania tu bali Afrika nzima.
Pamoja na kuibuka mshindi kwenye msimu wa pili wa shindano hilo na kuingia kwenye filamu, Richard ameendelea kuwa na maisha low profile ambayo kwa namna yoyote ushawishi wake ni mdogo. Pia kama Mwisho Mwampamba angeendelea na spidi aliyokuwa nayo, alikuwa na nafasi kubwa ya kusonga mbele zaidi muda huu. Muonekano wake ni dhahabu aliyoamua kuichezea mchangani.
Tatizo lingine kubwa la mastaa hao ni kutoitumia mitandao ya kijamii kujiweka karibu na mashabiki na kuwa pia ‘available’ kwa michongo ya kimataifa. Twitter ama Facebook siku hizi imekuwa kama daraja la mawasiliano kati ya mashabiki au makampuni na staa. Ni sehemu ambayo mashabiki hujua kile kinachofanywa na mastaa wanaowapenda.
Kidogo Elizabeth ameweza kuzitumia fursa alizozipata baada ya BBA ambapo licha ya kuolewa Kevin Pam wa Nigeria aliyekuwa mshindi wa msimu wao, ameweza kujipenyeza kwenye ulimwengu wa filamu za Nigeria na ana nafasi nzuri ya kung’ara.
jpg
The Cartel, filamu aliyoigiza Elizabeth
Lotus, Bhoke, Hilda na Julio tayari wamesahaulika haraka hasa kwakuwa hawakufanya vizuri kwenye misimu yao. Hata hivyo Julio ameendelea kutafuta fursa nyingine kwa kufanya hip hop japo bado hajatoka.
Feza Kessy na Ammy Nando ni story tofauti kabisa. Licha ya kwamba hawajaweza kufika fainali, wanaonekana kama washindi kwa namna wanavyopendwa na jinsi walivyo na ushawishi mkubwa barani Afrika kwa sasa. Story yao ni mafanikio, kupendwa na kushawishi.
Nando anaongoza kwa kuwa na ushawishi zaidi kwa sasa ambao unaonekana wazi kwenye akaunti yake Twitter. Tumeshaanzika habari kadhaa za jinsi wasichana wengi wa Afrika wanavyopigana vikumbo kuliwinda penzi lake.
Nando ameweza kuwashawishi vijana wengi kwenye maisha yao ya kila siku kwa mfano namna ya kuishi maisha halisi na kujiamini. Hii ni mifano ya jinsi Nando alivyo na ushawishi katika maisha ya watu.
Zamathembu Mthembu:
Thank u for reminding us to value friendship,to be honest nd to never backstab friends for the sake of money.
Ruth Mafonki Montsho
Ammynando i love u cos u teach me to speak my mind always I can’t wait too see u again.
Tangu atangaze kuanzisha nguo zake ‘Brotherhood’ mashabiki wake wanahisi anachelewa kuziingiza mtaani ili wazinunue. Kwa namna ambavyo zinasubiriwa kwa hamu, nguo zake zitafanya vizuri sana sokoni.
BR2XuESCUAAGay2
Nguo za Nando, Brotherhood
Kwa namna ambavyo Nando amejikusanyia mashabiki, kila kitu atakachochagua kufanya kitafanya vizuri. “We cnt wait man, da industry need ur intelligence en will support,” alitweet shabiki wa Nando baada ya Nando kutangaza kuwa amemaliza likizo yake na yupo tayari kuingia kazini.
Nando ameingia Big Brother akiwa na followers si zaidi ya 4,000 lakini tangu atoke, akaunti yake imeendelea kukua kwa haraka na sasa anakaribia kufikisha followers 15,000.
Kwa upande wake Feza, picha za mapokezi aliyoyapata nchini Botswana zinaonesha wazi jinsi anavyokubalika.
BSIhBhlCEAAAXBU
Mapokezi hayo yamemshangaza yeye pia na kujiuliza ni kipi alichokifanya hadi apendwe kiasi hicho.
“I’m still overwhelmed by Botswana. I’m in shock; I don’t know what I did yo. I’m speechless. I thank you & ke a le rata,” alitweet. Hiyo ni ishara kuwa, future yake kimuziki ni nzuri na ana uhakika wa kuwa mwanamuziki mkubwa iwapo ataendelea kufanya muziki mzuri.
Tunaamini Nando na Feza watafika mbali na watafanikiwa sana.
Previous Post Next Post