Kampuni ya Apple watengenezaji wa simu aina ya iPhone imesema itafanya uchunguzi juu ya madai ya mwanamke mmoja wa China aliyedaiwa kupoteza maisha kwa kupigwa shoti wakati akizungumza kwa simu yake ya iPhone aliyokuwa anaicharge.
Madai hayo yamewasilishwa na msichana kutoka magharibi mwa China Xinjiang, aliyeandika barua kwa mtandao maarufu wa China ‘Sina Weibo’ kuelezea kilichomsibu dada yake mkubwa Ma Ailun aliyekuwa na miaka 23.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, polisi wamethibitisha kifo cha msichana huyo kimetokana na shoti ya umeme, lakini haijathibitishwa bado kama simu yake ilihusika.
Msemaji wa Apple nchini China Carolyn Wu amesema wanafanya uchunguzi juu ya tukio hilo na pia akatoa pole kwa familia ya marehemu. “We will fully investigate and cooperate with authorities in this matter,” Alisema.