BBA The Chase: Kenya hatarini tena, Annabel apata kura nyingi za kutoka!



Inavyoonekana nyumba ya Diamond katika jumba la ‘kaka mkubwa’ ina nuksi kwa mshiriki wa Kenya Annabel ambaye jana tu (July 14) ameokolewa na kura za Tanzania, Uganda na Kenya na kubakia katika Tha Chase, leo tena amejikuta anapata kura nyingi za kurudi tena dangerzone wiki hii.
Annabel2
Annabel na Bimp wa Ethiopia ndio wameongoza kwa kura za leo kuingia dangerzone kwa kupata kura nne kila mmoja, kura ambazo hupigwa na washiriki wote katika nyumba zote mbili Diamond na Ruby kwaajili ya kupata washiriki watakaoingia dangerzone itakayoamua wawili kati yao kuondoka mjengoni jumapili katika eviction show.
Hivi ndivyo kura zilizopigwa leo Diamond house ikionesha kila mshiriki alivyowapigia kura za kutoka wenzake:
Annabel: Beverly and Bimp
Bimp: Annabel and Dillish
Bassey: Bimp and Annabel
Nando: Melvin and Dillish
Beverly: Annabel and Bassey
Dillish: Bimp and Nando
Melvin: Bimp and Annabel
Previous Post Next Post