Odama awajibu wanaomtuhumu huzifanyia ‘photoshop’ picha zake na kudanganya alikuwa Ulaya



Baada ya kuzagaa kwa habari zikimtumu mwanadada wa filamu Tanzania Jennifer Kyaka aka Odama kwamba huzifanyia makeke ya photoshop picha zake na kuwadanganya wananchi kuwa amezipigia Ulaya, ameongea na Bongo5 kukanusha huku akionesha picha halisi zinazomuonesha akiwa mbele.
IMG-20130715-WA0006
Baada ya tuhuma hizo kumkabili Odama, Bongo5 ilimtafuta mwanadada huyo wa filamu na ndipo alipokanusha tuhuma hizo na kusema hakufanya kitu kama hicho na kwamba waliosema hivyo wanania mbaya naye.
Ili kukata ‘ngebe’ za manisnitch hao Odama ametutumia bongo5 picha hizi za ushahidi kwamba alikuwa nje ya nchi kama alivyosema.
“Kuna watu wanakosa vy kufanya ndio maana wanakaa na kuanza kuzusha vitu ambavyo hawana uhakika navyo so siwashangai kwakuwa binadamu tunatofautiana upeo,” ameiambia Bongo5.

IMG-20130715-WA0004

IMG-20130715-WA0005
IMG-20130715-WA0003

news via : bongo5
Previous Post Next Post