Shilole ndani ya beef la "kifo" na Sintah, kisa? Soma hapa





Mwigizaji wa bongo movies na mwanamuziki wa kizazi kipya Zuwena Mohamedi ama shilole ameingia katika beef la hatari na mwigizaji, blogger na mtangazaji wa kituo cha DTV Christine Sintah “Sintah”

CHANZO NINI?

Habari zinasema kuwa tatizo limeanza baada ya Sintah kuandika kwenye blog yake kuwa mwanadada Shilole kuwa hana Kipaji cha kuimba kama tunavyonukuu maneno yake hapa chini…
“…sasa J wake Lo na Shilole jamani hebu tuweni wakweli aiiiii nimesema kidogo kwa Lina anyway tusubiri collabo nahisi nitaenda kuingiza vocal maana my dada hatokosa kuniita nijionee mchiriku mix…”

SHILOLE AMJIBU…

“Nashangaa, sijawahi kumuona mwanamke mwenye roho dhaifu kama Sintah, anajifanya anambabaikia Jlo wakati hata hajulikani, ameshangaa watu wa Bongo kuwa na tabia ya kudharau muziki wa nyumbani na kubabaikia muziki wa Marekani wakati wenyewe hawana muda muziki wa hapa Bongo, anamchukia Sintah kwa kuongea kitu asichojua na kumponda yeye na Snura…”
“Mimi sikuwa nimeenda Marekani kwa ajili ya kuomba kumshirikisha J-lo kuimba naye lakini baada ya meneja wake kuja kuniona na kumpelekea video za muziki wangu alikubali kufanya kazi na mimi, ilitakiwa nionane naye siku ya Jumapili lakini ndio siku niliyoondoka na ninarudi huko kwa ajili ya kazi hiyo, sijui nikifanya naye kazi atajificha wapi?,” anasema Shilole….
Shilole anasema Mungu ni mkubwa hata kama kuna mtu anayemchukia kwa mafanikio yake bado Mungu ana nafasi kubwa kuwazima watu wenye roho mbaya wivu kama Sintah ambaye anaonekana yupo tayari kwa ajili ya kuwaombea matatizo watu wanaojituma kwa ajili ya kuendesha maisha yao.

AAPA KUMPA KIPIGI CHA MBWA MWIZI AKIMUONA

Kama maneno hayo hapo juu hayatoshi shilole ameapa kumpa sintah kipigo cha kufa mtu akimouna..
“Ni kweli sisi wanawake hatupendani na kuwa na wivu wa kijinga, mtu anakurupuka anakotoka bila hata kufanya utafiti na kunibeza eti sina uwezo wa kuimba na JLO (Jenifer Lopez) kuna mtu aliyetegemea mimi kwenda kufanya show Marekeni! Sasa ninachomwambia ninamtafuta nikikutana naye nimtapa kipigo cha Mbwa mwizi,”aliongea kwa hasira Shilole….
Nini kitafuatia? Yetu macho….tupe maoni yako...
Previous Post Next Post