RAIS JAKAYA KIKWETE AMEMTEMBELEA MMILIKI WA HOME SHOPPING CENTER ALIYEMWAGIWA TINDIKALI (ACID)


Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtembelea “Said Mohamed Saad” ambaye ni mfanya biashara na mmiliki wa home shopping center.


Mfanyabiashara huyo alimwagiwa tindikali na mtu mmoja ambaye hakufahamika na mara baada ya kutenda tukio hilo, mhusika alikimbia huku mlinzi wa eneo hilo akijaribu kumkimbiza pasipo mafanikio

Rais Jakaya Kikwete alisema “Ameungua sana, tunatarajia kati ya kesho au keshokutwa (wikiendi iliyopita) atafanyiwa oparesheni ya jicho. Jamani tindikali ni mbaya sana, usimmwagie mwenzako. Ndugu yetu ameharibika sana,”
“Kila anayemjua vizuri, anapomwona anamwaga machozi. Picha za jinsi alivyoathirika baada ya kumwagiwa tindikali zimevuja mpaka kwa familia, ni kilio kwa ndugu.”
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA