Ostaz Juma na Musoma (Watanashati) aingia kwenye ‘Hip Hop’ amshirikisha Young Killa


Fid Q na rappers wengine kaeni chonjo!! Mmiliki wa lebo ya Watanashati Entertainment, Ostaz Juma na Musoma ameingia studio na kurekodu ngoma ya Hip Hop iitwayo ‘Muziki Kazi’ aliyomshirikisha Young Killer.
Akiongea na Bongo5, Ustaadh amesema wimbo huo ameurekodi jijini Mwanza kwenye studio za K Records.
“Nilienda studio ya K Record ya Mwanza nikamkuta Young Killer ndipo tukapata wazo tufanye kitu ,tukaanza kukusanya mawazo mpaka tukaanza kuimba, ndipo siku iliyofuata tukaamua kurecord. Kwakweli haikuwa kazi rahisi kuweza kurecodI kwani Young Killer amenifunika kwakuwa ni mzoefu ila nawaambia wale ambao wanadharau kazi ya muziki wajaribu kuingia studio ili waone muziki unakuwaje.”
Ostaz amesema wimbo huo utatoka baada ya mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan na atauachia kwenye internet peke yake.
Msikilize zaidi hapa.

Previous Post Next Post