SOS B sasa hivi ni producer wa muziki, anatarajia kuachia ngoma mpya

Hasikiki tena kwenye mawimbi ya radio, lakini Sosthenes Ambakisye aka SOS B hawezi kusahaulika kwa heshima aliyoiacha kwenye industry mbili muhimu nchini, Utangazaji na Hip Hop.
SOS B aliyekuwa akijulikana pia kama ‘Kalikamo’ ni miongoni mwa wahasisi wa rap ya Tanzania na uwezo wake ulipelekea apate tuzo ya wimbo bora wa hip hop wa mwaka 1996 kwa hit single yake ‘Kukuru Kakara Zako.


SOS B pia ni miongoni mwa watangazaji mahiri kabisa wa vipindi vya burudani kuwahi kutokea nchini Tanzania na hakuna anayeweza kusahau vipindi vyake alivyokuwa akivifanya kwenye kituo cha Radio One.
Rapper na mtangazaji huyo ambaye aliwahi pia kushirikishwa kwenye hit single ya Profesa J, ‘Piga Makofi’ anakumbukwa kwa umahiri wake wa kutengeneza jingle za radio kwa sauti yake mwenyewe.
Hivi karibuni kupitia Facebook aliandika:
ANNOUNCEMENT..Guys I do music remixes…what I need is only your Accapela/Vocals to make it happen…BONGO FLAVA where u at.”
Na mwa mujibu wa blog ya Dj Fetty, huenda SOS B akarejea tena na ngoma mpya. Blog hiyo imeandika:
Mmiliki wa ngoma hiyo Rapper Sos B, anajipanga tena kuachia dude jipya litakalotengenezwa na studio yake mpya, huku yeye mwenye aki-produce ngoma hiyo.
Inawezekana Sos B alikuwa akifanya majaribu kuona kama anaweza kurudi, kwasababu nimekutana na demo yake ikiwa imevuja kwenye mtandao, akisikika akichana mistari aliyowahi kuichana katika wimbo wa “Piga makofi” ya Prof Jay.
Kwa sasa SOS B ni baba wa watoto wawili.
Previous Post Next Post