Mabeste ajibu swali muhimu lililokuwa likiumizwa vichwa vya wengi



Rapper wa B’Hits, Mabeste leo ametoa fursa kwa mashabiki wake kumuuliza maswali kupitia ukurasa wa Facebook. Miongoni mwa maswali muhimu yaliyoulizwa na ambayo watu wengi wamekuwa wakijiuliza pia ni pamoja kuhusu uraia wa wazazi wake na shughuli anayoifanya zaidi ya muziki.
394344_317607995005127_21993806_n
Akijibu swali kuhusu wazazi wake, Mabeste Venance amesema baba yake ni Mtanzania huku mama yake akiwa Mkenya.
Pia amesema licha ya kufanya muziki, amekuwa akijihusisha na biashara na kwamba wimbo wake ujao baada ya ‘Dole’ unaitwa Are You Like Now’
Previous Post Next Post