Kutoka Big Brother The Chase: Nando adai alilazimishwa na Selly kufanya mapenzi ‘pasipo kinga’ na Selly kumwambukiza gonjwa la ngono



Mmoja wa wawakilishi wa Ghana kwenye msimu wa 8 wa Big Brother Africa, Selly aliyaaga mashindano hayo siku kadhaa baada ya mwakilishi wa Tanzania, Ammy Nando kumshutumu kuwa amemuambukiza ugonjwa wa ngono (STD) pindi wawili hao walipoamua kujamiiana ndani ya jumba hilo.
546624_324919007586612_369082865_n
Nando ameendelea kuchukizwa na ukweli kuwa ameambukizwa gonjwa hilo na amekuwa akiwaeleza washiriki wenzake bila kuficha.
“Unajua namchukua sana mal**ya huyo. Nimechanganyiwa sababu mal**ya huyo amenipa STD. Ndio maana jana blood pressure ilikuwa juu sana,” alimwambia Methiopia Bimp.
Kwa mujibu wa Nando, alitaka kutumia condom kabla ya kufanya mapenzi na Selly, lakini msichana huyo alikataa na kudai alitaka wafanye pekupeku na Nando kujikuta akikubali bila kujua angeambukizwa.
EvictedProfile_0020_74d1aab9-1a24-4e1d-bbad-f477f8add475_571314205712711
Ripoti zinadai kuwa madaktari wanaendelea kumtibu Nando ugonjwa huo wa Chlamydiae. Hata hivyo hakuna ushahidi kuwa Nando aliupata kwa Selly.
Mapenzi hayo kati ya Selly na Nando yalikuwa habari kubwa nchini Ghana kwasababu msichana anafahamika kuwa na uhusiano na Steven Fiawoo aka Praye Tiatia.
Mama yake Selly, Benedicta Galley amekiambia kipindi cha Entertainment Review cha Peace FMkuwa huenda Nando alitumia ‘juju’ kwa binti yake kwakuwa amemlea kwenye maadili mazuri na amekuwa na uhusiano Praye Tiatia kwa zaidi ya miaka minne.
Previous Post Next Post