Mwimbaji mkongwe wa R & B kutoka Marekani Robert Kelly aka R.Kelly anategemewa kusuuza nyoyo za mashabiki wake wa Tanzania baada ya kuthibitisha kuja kutumbuiza nchini mwakani (2014) katika pambano la ndondi litakalomhusisha bondia mkongwe wa MarekaniEvender Holyfield hapa nchini.
Kwa mujibu wa promota Jay Msangi wa Hall of Fame boxing, mfalme huyo wa R&B R. Kelly amethibitisha kuwa atakuja nchini kutumbuiza mwakani (2014) na hivi sasa wako katika hatua za mwisho kukamilisha mipango hiyo.
“Kutakuwa na pambano Kati ya Evander Holyfield vs Francois Botha katika uwanja wa Taifa mwakani 2014 na R.Kelly atatumbuiza. We are working on finalize that deal. Evander and Botha wameshasini mikataba yao, R.Kelly mngment wamekofirm lakini bado hatujapata signature yake kwenye contract zetu, but we are working hard to finalize it very soon,” Msangi ameiambia Bongo5.
Msangi amesema R. Kelly atatumbuiza katika pambano kubwa la ndondi kati ya Evender Holyfield kutoka Marekani na Francois Botha wa Afrika Kusini katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, ambalo mwanzo lilipangwa kufanyika (April) mwakani lakini sasa linategemewa kufanyika mapema zaidi ya tarehe iliyopangwa awali.
Hata hivyo Bondia wa Afrika Kusini Francois Botha anategemewa kutua Tanzania mwezi (August) mwaka huu kwaajili ya kuanza kufanya uhamasishaji wa pambano hilo kubwa ‘epic boxing event’ na pia kuhudhuria pambano lingine kubwa kati ya bondia wa Tanzania Francis Cheka na mmarekani Derick Findley ambalo litakuwa la kihistoria kwa bondia wa Tanzania kupigana na mmarekani katika ardhi ya bongo.
Sehemu ya habari hii chanzo ni: DSTV