ETI!!!! Wema amzaba makofi meneja wa hoteli, kisa??? Pombe





Katika habari iliyoripotiwa kupitia mtandao wa Global publishers inasema kuwa mlimbendwe wetu wa bongo movies Wema Abrahamu binti Sepetu anatafutwa na polisi kwa kumzaba vibao mmiliki wa hoteli moja jijini dar es salaam alipoenda kula ‘bata’ weekend iliyopita.
Habari hiyo iliyoripotiwa na waandishi Mwaija Salum na Denis Mtima inasema kuwa…
DIVA wa filamu za Bongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu anasakwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Kawe, Dar es Salaam kwa tuhuma za kufanya fujo hotelini, kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga makofi meneja wa hoteli hiyo, Godluck Kuyumbu. Songombingo hilo lilijiri saa tano usiku wa Jumatano iliyopita kwenye hoteli hiyo (jina tunalo) iliyopo Kawe Beach, jijini Dar.
MAELEZO YA MENEJA
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, meneja huyo alisema siku ya tukio majira ya saa nane mchana, Wema alifika kwenye mgahawa wa hoteli hiyo akiwa ameongozana na marafiki zake wapatao kumi.

Chanzo ni wema na  wenzake kuzidiwa na kilevi...
Meneja huyo akaendelea kusema, ilipofika  saa tano usiku, Wema na marafiki zake  walionekana kuzidiwa na kilevi, wakaanza kufanya fujo kwa kupiga kelele, kitendo kilichowakera wateja waliokuwa katika mgahawa huo, wengi wakiwa ni Wazungu ambao waliondoka kutokana na fujo hizo.
Aliongeza kuwa mmoja wa marafiki wa Wema ambaye ilidaiwa ni mpenzi wake, aliyejulikana kwa jina moja la D, alichukua glasi na kuipasua chini kwa makusudi huku meneja huyo akishuhudia.
Meneja akasema: Wakati wanaondoka, nilimfuata yule jamaa mpaka nje, nikamuuliza ni kwa nini amevunja glasi kwa makusudi, akanijibu kwa dharau huku akinitukana na kutishia kunipiga, akawa ananiuliza hiyo glasi ni shilingi ngapi kwani? N baada ya hapo alitoka kwenye gari na kuanza kumlamba vibao visivyo na idadi meneja huyo huku akimpa maelekezo kwamba akashitaki popote na hawezi kufanywa kitu kwani yeye ana nguvu kwenye nchi hii.
“Niliamua kupiga simu Kituo cha Polisi Kawe, wakaja kuangalia mazingira kisha nikaondoka nao kwenda kufungua kesi kituoni.”
Faili la kesi hiyo linasomeka KW/RB5988/2013, SHAMBULIO. Hadi tunakwenda mitamboni, Wema anasakwa na polisi ili apandishwe mahakamani.

Majaribio ya kumpata mwanadada huyu kuthibitisha habari hizi hayakudhaa matunda kwani simu yake ya mkononi ilikuwa haipatikani muda wote tuliojaribu kumpigia.

-Habari kwa hisani ya mtandao wa Global publishers | waandishi-  Mwaija Salum na Denis Mtima-
Previous Post Next Post