Bond Bin Suleiman na Lulu wawa vinara kwenye Tamasha la filamu la ZIFF 2013.




Mtangazaji wa Televisheni ya Channel Ten ambaye pia ni mwigizaji wa filamu na mtayarishaji wa filamu, Bond Bin Suleiman usiku tuzo za Ziff alikuwa ndio nyota kwa usiku huo ambapo alishinda tuzo nyingi na kutisha katika tuzo hizo baada ya filamu aliyoiongoza Lover’s Island kunyakua tuzo tatu kwa mpigo, filamu hiyo aliyoigiza na wasanii wengine nyota kama Richard wa Big Brother iling’ara katika viwanja vya ngome Kongwe.
“Nimekuwa mwigizaji bora na mwongozaji bora na Lulu amekuwa mwigizaji bora wa kike kupitia filamu ya Women of Principal. Kwahiyo tunawashukuru wale waliotuchagua na kuona ubora wa kazi zetu na tuna wahaidi Watanzania kufanya mambo makubwa zaidi katika filamu.” Alisema Bond
Bond alijipatia tuzo ya kwanza kupitia filamu hiyo ya Lover’s Island akiwa kama mwigizaji Bora wa kiume, tuzo ya pili alishinda kama muongozaji bora wa filamu hiyo huku pia filamu hiyo ikichaguliwa kama filamu bora kwa mwaka wa 2012/2013 na kuufanya usiku huo kuwa wa Lover’s baada ya kuibuka na tuzo kibao.
Kwa upande wa akina dada naye mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ aliibuka kama mwigizaji bora wa kike kupitia filamu ya Woman of Principal akitumia jina la Linda, usiku huo ulichangamka kwa kushuhudiwa na mamia ya wakazi wa Zanzibar na wageni kutoka nchi mbalimbali, baada ya kushuhudia tuzo baadae walijumuka kwa kucheza muziki katika ukumbi wa Mambo Club huku Kassim Mganga akiwaburudisha waliofika katika viwanja vya Ngome Kongwe.

Previous Post Next Post

Popular Items