DROGBA KUJENGA HOSPITALI TANO KWA AJILI YA WANAWAKE NA WATOTO, IVORY COAST


drogba a96b3
KUPITIA taasisi yake ya kutoa misaada, nahodha wa Ivory Coast na gwiji wa Chelsea Didier Drogba atasaidia ujenzi wa kliniki tano za watoto na wanawake katika nchi yake. Tangazo hilo lilitolewa na katibu mkuu wa Didier Drogba Foundation Guy Roland Tanoh, ambaye alisema kwamba ujenzi wa kliniki hizo utafadhiliwa na Taasisi ya London galas pamoja na fedha Drogba mwenyewe. (HM)  
Tanoh amesema kiasi cha 2.5 billion CFA francs ($5 million) kitatumika kuwekeza katika ujenzi wa kliniki hizo, huku zikijengwa katika miji mitano mikubwa ya nchi hiyo Abidjan, Yamoussoukro, Man, Korhogo na San Pedro.
  “Drogba aliendesha mchango huko London na zikapatikana kiasi cha $ 2 billion CFA francs ($4 million),” Tanoh alisema. “Kiasi kilichobakia cha million francs ($1 million) hakitakuwa tatizo kuona ndoto ya mwenyewe Drogba ya kuona afya za wananchi wa Ivory Coast zinapewa kipaumbele.”
 Drogba mara ya kwanza alitangaza mpango wake wa kujenga hospitali kubwa katika jiji la Abidjan mwaka 2009 akitumia fedha zote - kiasi cha £3 million ($4.5 million) alicholipwa na Pepsi. Lakini badala ya kujenga hosptali hiyo moja kubwa akaamua ambayo ingekuwa mjini tu, akaamua kujenga vituo vitano vya afya katika mikoa mingine ili kuweza kusambaza vizuri huduma za afya. 

news via: Supersport
Previous Post Next Post