Mikataba ya kuchimba dhahabu hapa nchini ilianza kusainiwa na serikali ya awamu ya tatu ya Mzee Benjamen William Mkapa; mikataba hii imesainiwa katika taratibu na mazingira ya kifisadi kwa vile kwanza muda wa mikataba ni miaka 99 na murahaba wa asilimia tatu (3%), mikataba ya aina hii haipo popote pale duniani zaidi ya hapa kwetu Tanzania! Sasa mimi najiuliza kwamba hivi Mkapa alikuwa anafikiria nini kusaini mikataba ya asilimia tatu tena kwa kipindi cha miaka 99 wakati alikuwa anajua kwamba yeye amechaguliwa kwa kipindi cha...
miaka 10 tu! Je, alijiona kwamba amepata wawekezaji wajinga sana kiasi kwamba wamekubali
kutoa asilimia tatu hivyo aliona akiwaachia hawawezi kupatikana tena!? Na ndiyo maana akaona
madhali wamekubali kusaini mikataba basi asiwape nafasi bali awagandamize kwa kuwapa
mikataba ya miaka 99! Mimi ninavyooona hata hiyo asilimia tatu hatuipati kulingana na hali
halisi ya ufisadi uliopo hapa nchini, kama kuna kitu tunachopata kutoka katika mikataba hii
ya kifisadi ya dhahabu haiwezi kuzidi nusu asilimia kwa mwaka (0.5%)! Ni kwanini Mkapa
asingelisaini mikataba hata ya zero point one percent (0.1%) lakini iwe mkataba wa miaka 10 tu!
Tukiachana na mambo ya asilimia (murahaba) ambayo nitayachambua baadae katika makala
hii, ningependa nijaribu kuzungumzia hujuma zinazofanywa katika migodi yetu; migodi yetu
ya dhahabu inafanyiwa hujuma ambazo huwezi kuamini kama nchi hii kweli ina wenyewe, na
hata kama wapo wenyewe lakini hawapo hai bali watakuwa wameshakufa! Nasema hivyo kwa
vile kulingana na taratibu za uchumbaji wa madini duniani, hasa tukijifunza kutoka kwa nchi
kiongozi wa uchumbaji wa madini duniani ya Afrika ya Kusini; mgodi wa madini ya aina yoyote
ile ni lazima uwe umeajiri wafanyikazi ambao hutekeleza majukumu mbali mbali katika mgodi
huo kulingana elimu au ujuzi waliokuwa nao, hawa wote ni wafanyikazi ambao wanautegemea
mgodi huo kwa ajili ya kupata mishahara na kutunza familia zao; baadhi ya wafanyikazi ni
vijana ambao hawana familia na wengine ni watu wazima ambao wana familia zinazowategemea
ikiwa ni pamoja na kusomesha watoto, matibabu, kuwalisha na kuwavalisha, hivyo jinsi
shughuli za mgodi zinavyodumu kwa muda mrefu ndiyo ambavyo wafanyikazi wanavyoishi
maisha mazuri ikiwa ni pamoja na kuzimudu familia zao. Kwa serikali yoyote ile makini lazima
ihakikishe kwamba inalinda ajira za wananchi wake kwa kuhakikisha kwamba umri wa mgodi
unadumu kwa muda mrefu kadri inavyowezekana ili kuendelea kutoa ajira kwa wafanyikazi
waliopo kwenye mgodi huo na wale wapya wanaoajiriwa kila mwaka,na hii inawezekana tu kwa
kuhakikisha kwamba serikali inawadhibiti hao wanaoitwa wawekezaji wasivuke viwango wa
uchimbaji udongo vilivyowekwa na taratibu za kimataifa za uchimbaji madini.

Nasema hivyo kwa vile machimbo yetu ya dhahabu yamekuwa yakihujumiwa sana na hawa
wanaoitwa wawekezaji kwa vile wanachimba madini kwa fujo ili kwamba yaishe haraka
haraka kama vile wametaarifiwa kwamba wenyewe wamelala hivyo jitahidini mchimbe kwa
haraka kwa vile wakiamka tu basi watawafukuza; maneno haya ni sahihi kwa vile udongo
unaochimbwa kwa siku moja kwenye machimbo yetu ya kule Geita na Bulyankulu ni udongo
ambao unachimbwa kwa mwezi mmoja kule kwenye machimbo ya Afrika ya Kusini au Ghana;
sasa hii inaonyesha kwamba tunafupisha maisha (life span) ya migodi yetu kwa mara thelatini;
ina maana kama mgodi ungedumu kwa miaka 90 basi inabidi mgodi huo udumu kwa miaka 3
tu! Sasa dhahabu ikiisha haraka kiasi hicho wafanyikazi wanaotegemea mgodi huo wataenda
kufanya kazi wapi au wataishi vipi wakati kazi itakuwa imeisha na wanategemewa na watu
mbali mbali katika familia zao? Mwaka jana nikikutana na Mine Engineer mmoja wa kutoka
Ghana ambaye alikuja hapa nchini kwa muda mfupi kwa shughuli hizo hizo za madini, hata
yeye alikuwa anashangaa kwamba kiasi cha udongo kinachochimbwa kwa siku ni kikubwa sana
kiasi kwamba kinahatarisha maisha ya wafanyikazi Wakitanzania wanaotegemea sekta hiyo
ya dhahabu; hii inaonyesha wazi kwamba serikali haipo makini na tatizo la ajira hapa nchini
licha ya kwamba viongozi, wanasiasa, wabunge na wanaharakati wamekuwa wakipiga sana
makelele kuhusu tatizo la ajira hapa nchini; ni kwanini wahubiri na mawakili wa bomu la ajira
kama akina Edward Lowasa wasitumie muda wao kwenda kwenye migodi yetu na kuyahimiza
makampuni yanayochima madini yapunguze kiwango cha udongo kinachochimbwa kwa kila
siku ili kuongeza muda wa maisha ya migodi yetu na wakati huo huo wakiwa wanalinda ajira
zilizopo na ajira mpya zitakazopatikana kulingana na kudumu kwa migodi hiyo.

Pamoja na kwamba serikali inajua kwamba taifa linakabiliwa na tatizo kubwa la macroeconomic
(kukua kwa uchumi, mfumuko wa bei, na ajira) lakini inaonekana kama hilo siyo tatizo lake,
serikali inadhani tatizo la macroeconomic ni tatizo la wananchi wenyewe, kitu ambacho siyo
sahihi kabisa; serikali nyingi duniani zimeondolewa madarakani na wananchi wenye hasira
hasa baada ya kushindwa kumudu hali ya macroeconomic ya nchi; nikizungumzia sekta ya ajira
serikali imeshindwa hata kuzilinda ajira zilizopo kwenye migodi yetu ili zidumu kwa muda
mrefu na pia kuhakikisha kwamba migodi hiyo inadumu kwa miaka mingi ili iendelee kutoa ajira
kwa vijana wa Kitanzania. Kulingana na ushahidi huu inaonekana serikali ina njama za siri na
makapuni yanayochimba madini hapa nchini kwa vile pamoja na kulipwa asilimia ndogo kuliko
wote duniani, lakini bado serikali inaonekana imewafumbia macho wawekezaji hawa matapeli
ambao wanachimba dhahabu kwa fujo kama vile wanaiba, jambo ambalo linajenga mazingira
hatarishi kwa ajira za Watanzania katika kipindi kifupi kijacho. Serikali yetu imekuwa ikfanya
mambo kijeuri kwa kutojali hatima ya ajira za Watanzania kwa vile Watanzania hawana desturi
na mila za kuzipumzisha serikali sisizowajibika kwa raia wake; majirani zetu kule Zambia
serikali inapumzishwa kwa mfumuko wa bei tena si asilimia thelathini (30%) kama sisi hapana,
Zambia serikali yaweza kupumzishwa kama unga unapanda bei kwa centi kumi tu! Hivyo
kulingana na hali hiyo serikali za wenzetu zinawaogopa na kuwatii wananchi wakijua kwamba
wao ndiyo waajiri wao, hapa kwetu sisi ndiyo waajiri wa serikali lakini wao wametugeuka sisi na
tumekuwa watumwa wao!

Tukirudi kule kwenye migodi yetu ya dhahabu ni kwamba uchimbaji wa dhahabu hapa nchini
tangu umezinduliwa na serikali ya awamu ya tatu ya Mkapa imekuwa ni sekta ya siri ya hali ya
juu kama ilivyokuwa mikataba ya madini ya Almasi hasa kwa wananchi wa kawaida; mwaka
2007 wakati bado nilikuwa nafundisha kule chuo kikuu Mzumbe kuna mwanafunzi wangu
mmoja alipangiwa kufanya field kule Geita Gold Mine, alipofika huko hakupokelewa vizuri
kwa vile tangu siku ya kwanza tu alipoingia akajikuta hatakiwi kabisa kwenye maeneo hayo,
watu wote aliowakuta wakiwa ni Wazungu na Watanzania wote kwa pamoja hawamtaki, na
wakati wote wana wasiwasi na yeye kwamba asije akajayaona au akayajua yale ambayo hatakiwi
kuyajua mtu mwingine zaidi ya wale wananafanya kazi wa pale na wale wakubwa walioko
Dar es Salaam ambao hasa ndiyo wamiliki wakubwa wa migodi hiyo; pia mwanafunzi huyo
mara tu baada ya kufika mgodini hapo kilifanyika kikao cha dharura kwa wafanyikazi wote
isipokuwa yeye cha kuwatahadharisha kwamba wawe makini wasijisahau kwa kusema au
kumuachia mtu (mwanafunzi) huyo mgeni kujua siri za mgodi! Mwanafunzi huyu alifanya field
yake ya miezi mitatu akamaliza lakini hakujisikia kama Mtanzania kwa vile alibaguliwa sana
hata na wale ambao hawakustahili kufanya hivyo, na alipokuwepo huko alipata taarifa kwamba
Wazungu wanaogopa watu wageni kwa vile kwenye migodi hiyo wao wanahamisha utajiri wa
nchi hii wakishirikiana na watawala hivyo hawataki siri zao zijulikane kwa watu wa kawaida!
Sasa kama haya makampuni ya kuchimba dhahabu ni wawekezaji wa kweli ni kwanini wawe
wanawafanyia siri hata Watanzania ambao ndiyo wenye nchi!? Kama wanalipa kodi, na kama
kweli wanatoa hiyo asilimia tatu wanahofia nini tena!?

Katika kipindi cha utawala wa Mkapa kuna waziri wake mmoja wa madini na nishati aliwahi
kufanya ziara ya kikazi kwenye mgodi wa dhahabu wa Geita, alipofika mgodini hapo
alipokelewa shingo upande, akaruhusiwa kutembelea sehemu zote za mgodi ispokuwa alipofika
kwenye Ghala (Godown) ambalo ndipo yanapohifadhiwa yale matofali ya dhahabu akaambiwa
stop huko huruhusiwi kuingia! Akahoji kwanini siruhusiwi kuingia!? Kwani kuna nini cha
siri ambacho sitakiwi kukiona!? Mimi ni waziri wa madini hamuwezi kunizuia nisiingie
huko, lazima niingie! Makaburu wakamjibu tumeambiwa kwenye ghala asiingie mtu yeyote
mpaka tupewe idhini na bwana mkubwa; wale makaburu wakampigia simu Mkapa, Mzee
hapa yupo waziri wako wa madini tumemwambia umekataza mtu yeyote asiiingie huko lakini
hataki ameng’ang’ania amesema lazima aiingie! Je, tumruhusu au tusimruhusu? Mwacheni
aingie. Waziri alipoingia ndani ya ghala alianza kupiga mayowe baada ya kukuta ghala zima
limesheheni matofali ya dhahabu yamepangwa kuanzia chini hadi juu! Aliuliza kama dhahabu
hiyo inatoka wapi!? Alijibiwa kwamba inatoka mgodini hapo! Alistaajabu inakuwaje watu
ni masikini wakupindukia lakini nchi ina utajiri mkubwa wa dhahabu kiasi hicho! Pia alihoji
kwamba mbona hata hizo kodi za dhahabu hizo hajawahi kuziona!? Waziri aliporudi ofisini
kwake akataka aonyeshe uzalendo kwa kutaka kujua kwamba ile dhahabu ya matani kwa matani
aliyoiona kule Geita inaenda wapi!? Baada ya kuhoji hivyo akaonekana hastahili kuwa waziri
wa Tanzania akaondolewa na kupumzishwa moja kwa moja, na vijana wa kitengo cha usalama
wa taifa wamemuorodhesha kwenye kile kitabu cha maadui wa taifa, anaendelea kupata kibano
kama kawaida, na huku Watanzania wengine wakishabikia na kuona anavyotendewa ni sawa

na anastahili kumbe alikuwa anatutetea! Sasa mpaka hapo tu, bado hatujazinduka kwamba
machimbo ya dhahabu ni siri kubwa ya taifa, ambayo hatakiwi kuijua mtu yeyote ukiwaondoa
wale tu waliokula njama na makaburu!?

Tangu mwaka 1999 hadi leo nimekutana na kuongea na watu mbali mbali wanaojishughulisha
na uchimbaji wa dhahabu hapa nchini, pia nimeweza kusoma kwenye magazeti ya nchi za ulaya
nikagundua kwamba wawekezaji wote wa dhahabu hapa nchini wanalipa murahaba wa asilimia
thelathini (30%) na siyo asilimia tatu (3%) kama ambavyo watawala wanavyotuambia; maneno
haya nimeyathibitisha kwa kuongea na raia mbali mbali wakiwemo raia wa Australia, Canada
na South Afrika kwa vipindi tofauti. Sasa kama wawekezaji wanalipa murahaba wa asilimia
thelathini ni kwanini serikali iwadanganye wananchi kwamba ni asilimia tatu tu! Hiyo asilimia
ishirini na saba (27%) wanachukuwa akina nani na ipo wapi na imefikia kiasi gani tangu migodi
ifunguliwe hapa nchini!? Ni kwanini watu wachache wajinyakulie rasimali zote za nchi na huku
wakiwaacha wananchi wanakufa njaa!? Haya ni maswali muhimu sana kwa wananchi ambayo
wangependa wapate majibu yake haraka sana iwezekanavyo; wananchi wangependa kusikia
majibu haya yanatolewa na serikali bungeni ili yaweze kujadiliwa.

Rais Kikwete kabla hajawa rais naye mwenyewe alikuwa anaona kwamba asilimia tatu ni
ndogo sana, na alikusudia kuivunja mikataba hii ya dhahabu mara tu akipewa ridhaa ya
wananchi ya kuwa rais, kwa bahati nzuri amekuwa na alipoingia tu wananchi walimpigia
makelele kuhusu kuivunja mikataba ya Mkapa (Mr. Clean kama ambavyo watu wa usalama wa
taifa wanavyomuita!), akaanza kukwepa kuzungumzia swala hilo hadharani, na amejikausha
kama siyo yeye na ameshakula miaka yake nane amebakiza miaka yake miwili amkabidhi
kijiti mtu mwingine atakayeendelea kuilinda mikataba hiyo kwa mtutu wa bunduki kama
ambavyo inavyolindwa hivi sasa! Kwanini Kikwete anashindwa kuivunja mikataba ya kifisadi
ambayo bila hata ya kufanya udadisi wa kina inajionyesha wazi wazi kwamba ni mikataba
ya kuliangamiza taifa!? Kwanini hataki licha ya kwamba anaweza na ni kitu kidogo kiasi cha
kutamka na kila kitu kinabadilika!? Basi nawaomba kila mmoja wetu ajiulize kwanini!? Na
kwanini bunge liendelee kulinda mikataba ya kifisadi au bunge letu nalo lina matatizo!? Kwanini
wananchi tukae kimya kwa miaka mingi kiasi hicho wakati tunaona wazi wazi kwamba rasimali
zetu zinaporwa na watu wanaoitwa wawekezaji wakishirikiana na watawala wetu!? Kwanini
tuendelee kukaa kimya!? Kwanini serikali isione umuhimu wa kujiuzulu kwa vile imeshindwa
kulinda maslahi ya umma!? Je, wananchi wakichukua jukumu la kuiwajibisha serikali watakuwa
wamefanya makosa!? Kwanini wananchi wanatakiwa wafuate sheria, lakini serikali na watawala
hawafuati sheria!? Je, kila mtu akiamua kutokufuata sheria na kufanya afanyavyo tutaendelea
kuishi au tutaangamizana!? Je, hatuoni kwamba katika mazingira kama haya tunaharisha amani!?

Katika kipindi hiki cha kutafuta katiba mpya ya umma nimewasikia watawala wengi ikiwa ni
wale wastaafu na wale walioshikilia usukani wakisisitiza kwamba ni hatari rais kupunguziwa
madaraka, akipunguziwa madaraka eti atashindwa kuongoza, tena aongezewe madaraka ili
atawale vizuri!? Wale wote waliotoa maoni ya namna hii kwanza hawana utu, ni watu wakatili

sana, watu wabinafsi, watu wenye chuki na umma wa Kitanzania, pia ni watawala wababaishaji
wasiokuwa na malengo wala maono! Sasa katika mazingira kama haya tunayoyaona hapa, je,
rais aongezewe madaraka ili atufanyie nini kibaya zaidi ya hiki anachotuifanyia!? Kama nchi
zingine zote dhahabu inachimbwa kwa kugawana nusu kwa nusu, hapa kwetu tumedanganywa
kwamba ni asilimia tatu, kumbe ni asilimia thelathini! Bado wapambe wanataka rais aongezewe
madaraka, rais ambaye ameshindwa hata tu kutamka hadharani kwamba mikataba ya dhahabu ni
ya kifisadi! Sasa aongezewe madaraka afanye nini!?

Nchi za Uarabuni miaka ya nyuma walisaini mikataba ya kifisadi ya kuchimba mafuta na
serikali ya Ufaransa, walipoingia madarakani watawala wapya walivunja mikataba yote,
na wakabadilisha kiwango cha murahaba, Wafaransa wakazira na kuondoka, walidhani
Waarabu watawabembeleza, baada ya miaka mitano yale mafuta waliyokuwa wamejilimbikizia
kumaliza wakarudi kuomba kusaini mikataba mipya tena walirudi kwa adabu ya hali ya juu!
Hii iliwezekana kule Uarabuni kwa vile watawala wapya hawakutaka kuendeleza vitendo vya
ufisadi; sasa sisi hapa mbona tunashindwa kufanya hivyo!?

Pamoja na kwamba serikali imewafanyia hujuma nyingi wananchi juu ya rasimali nyeti
ya dhahabu kwa kuwadanganya kwamba serikali wanapata asilimia tatu kumbe ni asilimia
thelathini (30%), kwa kutotaka kuisitisha kwa kuivunja mikataba hiyo ambayo inaonekana wazi
wazi kwamba ni mikataba ya kifisadi, lakini pia serikali imekuwa na chuki kwa Watanzania
kwa kutokuweka mikakati endelevu ya kulinda ajira zilizopo na ajira tarajiwa kwa kuwaruhusu
wawekezaji matapeli kuchima udongo mwingi kwa siku moja ukilinganisha na idadi ya viwango
vya kimataifa, kitu ambacho kinafupisha maisha ya migodi ya dhahabu hapa nchini; pia serikali
haijatilia maanani swala la kuwarithisha Watanzania tekinolojia ya kisasa ya uchimbaji wa
dhahabu na madini mengine; tunachimba dhahabu ambayo miaka michache ijayo itakuwa
imeshaisha kama ambavyo Almasi ilivyoisha, na dhahabu ikiisha tutakuwa tumepoteza kazi na
biashara zote zilizokuwa zimesababishwa na kuwepo kwa madini hayo, hivyo kama tutakuwa
hata hatuna tekinolojia hiyo tutakuwa tumepoteza kila kitu kwa vile kama dhahabu itakuwa
imeshaisha lakini tuna tekinolojia tutaitumia know – how hiyo kuiuza kwa nchi zingine ambazo
kwa wakati huo wao ndiyo watakapokuwa wameanza kuchimba dhahabu yao; kama ambavyo
ilivyo South Afrika wana tekinolojia ya hali ya juu kuhusu madini hivyo hata madini yao
yakiisha, lakini bado wataendelea kulinda ajira zao na pia kupata pesa nyingi kwa kuwauzia au
kuzisaidia nchi ambazo zinazochimba madini kama sisi hapa Tanzania. Ikiwa akiba ya madini
ya dhahabu hapa nchini inakaribia kuisha na bado hatujafaidika na lolote kutokana na dhahabu
hiyo, na wala hatuna hata tekinolojia yoyote kwamba twaweza kwenda nchi yoyote hapa barani
Afrika kuwasaidia uchumbaji wa madini hayo kama wataalamu na tukapata ajira na pia pesa
inayotokana na know – how sasa tunafaidika vipi na madini haya!?

Mwaka 1970 Nyerere alipewa mkopo wa masharti nafuu na serikali ya Sweden ili amjengee
kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 nyumba ya kisasa yenye thamani ya shilingi milioni
20 za sasa hivi, yeye akasema siyo kila Mtanzania mwenye uwezo wa kukaa kwenye nyumba

ya kisasa, badala yake akazichukua pesa hizo na kufungua bank ya THB yeye na vijana wake
wakaifisadi, hadi leo kila Mtanzaniania analipa deni hilo bila ya kujali alishirikishwa kwenye
ufisadi huo au lah! Leo hii Kikwete na serikali yake ya CCM pamoja na kwamba tuna dhahabu
nyingi sana, lakini wanaona kwamba bado siyo muda muafaka kwa kila Mtanzania kuvaa kidani
au pete ya dhahabu, sawa hata kama mmeamua hivyo lakini hata kazi zetu nazo mmeshindwa
kuzilinda!? Dhahabu itaisha na itaondoka tutaachiwa mashimo na tutaisahau kama vile hakuwahi
kuishi hapa Tanzania, lakini kwanini iondoke na kazi zetu na hata isituachie hata tekinolojia
Know – How!? Ili na sisi siku moja tuitwe nchi zingine za Kiafrika tukawaibie kama ambavyo
makaburu wanavyotuibia hapa Tanzania!

Dr. Noordin Jella (Ph.D. in Economics)
Former Lecturer of Mzumbe, Open & KIU – Dar, Universities.
Currently: Freelance Journalist & Seasonal Political
Analyst
Email: norjella@yahoo.com
Mobile: +255 782 000 131

Tags:
Social