Msanii anayefanya vizuri sana kwa sasa Afrika mashariki Nasib Abdul aka Diamond Platnumz amezungumza maneno mazito aliyokiri huwa yanamtoa machozi, ni mambo yanayohusiana na ‘kifo chake’!.
Dakika chache zilizopita hit maker huyo wa ‘Kesho’ ame post picha Instagram yenye sura yake na maswali yanayouliza nini kitatokea baada ya kifo chake. Tazama picha hiyo inazungumza yenyewe
Picha hiyo ilisindikizwa na caption hii “One of my songs,always gets me crying whenever I listen to it, how I wish u would hear it, but then again I have no clue as to when I will release it… #WCB”
Platnumz amekaa kimya bila kutoa wimbo mpya kwa muda sasa, je unahisi kuna uwezekano‘KAMA NIKIFA KESHO’ ukawa ndio ndio wimbo mpya anaotegemea kuachia hivi karibuni? Tusubiri tuone!