Diamond na Fuse ODG Kuja na Hit Hivi Karibuni




Msanii wa kizazi kipya Nassib Abdul a.k.a Diamond Platnumz weekend hii ameonyesha picha akiwa na hitmaker wa Antenna, Nana Richard Abiona aka Fuse ODG wa nchini Ghana kiasi cha kutufanya tuhisi jamaa hawa wanapika kitu jikoni.
da63e85cf07011e2950722000a1fc86f_7
Diamond amepost picha kupitia instagram akiwa na mkali huyo wa Antena ,Fuse ODG na kuonyesha wawili hao wana lengo la kufanya kitu pamoja ilikuchanganya Bongo flava na Azonto kutoka Ghana.
Diamond aliandika “Let’s see what we can Get if we Mix #Bongoflavour from Tanzania and #Azonto from Ghana…. here wit maboy @fuseodg ..the ANTENA hit Maker..!”
Hata hivyo kama kutakuwepo na collabo hii si jambo la kushtua sana kwakuwa kampuni inayommanage Fuse ilionesha interest ya kumchukua pia Diamond na huenda mambo ya mikataba yameshakamilika.
Diamond amekuwa msanii mwenye mafanikio makubwa kutokana na kupata deal nyingi za show na matangazo. Mnamo tarehe 17 mwezi huu website moja maarufu ya Kenya “Ghafla” iliandika habari “Why Diamond is East Africa’s Biggest Crowd-Puller” na kudai kuwa umaarufu wake umeuzidi wa Jose Chameleone.
Previous Post Next Post