Albino Fulani: Nilitarajia wasanii wengi Tanzania wangempongeza Wakazi kwa kazi nzuri ya BBA Eviction Show


Rapper Babu Sikare aka Albino Fulani aishiye nchini Marekani ameiambia Bongo61 kuwa amesikitishwa na jinsi wasanii wengi wa Tanzania walivyoshindwa kujitokeza na kumpongeza Wakazi kwa performance kali aliyoitoa jana kwenye eviction show ya Big Brother Africa The Chase.
“Nilikuwa na matarajio makubwa zaidi, kwamba wasanii wakubwa watajitokeza na kuwa proud ya young new talent. Kabla kuna waliokandya, he did good na hapati credit stahili,” amesema Sikare.
Hata hivyo amekiri kuwa sio wote huiona show hiyo kwakuwa huonekana kwa wale walio na DSTV lakini amesisitiza, “Ila pia nimeona ma artist wakubwa wakibishana na kuonyesha kuwa ni wapemzi damu wa BBA. Basi hata kusema “hongera, nimesikia….”
“Kuna nyufa katika sanaa yetu. Ili tuendelee inabidi tuwe na ushirikiano ndani na nje ya studio tunapokutana. Tusijenge mioyo yenye Chuki, Wivu, kinyongo kati ya wasanii na wasanii. Ndio maana unasikia fulani karushiwa chupa kwa steji…. Tukiendelea namna hii kutakuwa na Makundi yatakayoua sanaa.”
Previous Post Next Post