Kundi la matapeli wanaojiita Saving Foundation leo wameihack akaunti za Facebook na Twitter za Diamond na kuandika ujumbe unaoonekana kama umeandikwa na Diamond.
Tumempigia simu na Diamond ambaye hakuwa na taarifa zozote kumuuliza kama ni yeye ndiye aliyeandika na amekanusha kuandika ujumbe huo.
Ujumbe huo kwenye akaunti ya Facebook ya Diamond unasomeka ivi:
Matapeli hao pia wamewahi kutumia majina ya Zitto Kabwe na Ridhwan Kikwete kufanya utapeli huo.
Mr Jr Botea ambaye ni Mtaalam wa masuala ya IT toka Aptech ameiambia Bongo61 kuwa matapeli hao wamejipanga na wana mtandao mkubwa Unaowawezesha wao kufanya kazi zao kwa uraisi zaidi.