NEWS ALERT: GHASIA KUBWA YATOKEA BAINA YA WANDAMANAJI NA POLISI HUKO MJINI INSTABUL,UTURUKI




Instabul,Uturuki: Baada ya maandamano ya wiki tatu katika mji mkuu wa Istanbul,nchini Uturuki, Mapema leo wandamanaji waliamrishwa kuondoka mara moja katika viwanja vya Taksim Square,Istanbul,amri hiyo ilitolewa na meya wa mji huo Bw. Huseyin Avni Mutlu.


Meya huyo aliwataka wandamaji waondoke katika viwanja hivyo ili usafi uweze kufanyika wa kusafisha eneo hilo,lakini wandamanaji waliendeleza libeneke la maandamano,Waziri mkuu wa nchi hiyo Bw.Tayyip Erdogan amekubali kuonana na viongozi wa maandamano hayo siku ya jumatano na kusikiliza matakwa yao,lakini kabla ya viongozi hao kuonana na waziri mkuu wa nchi hiyo.


Askari wa kutuliza ghasia (kina Ras makunja) wa nchi hiyo wameshavamia viwanja vya Taksim Square na kuwarushia wandamanaji milipuko ya machozi,maji ya kuwasha na mkong'oto kama ilivyo mila na desturi yao kina ras makunja(FFU).


Kwa Habari Zaidi bofya hapa http://www.abc.net.au/news/2013-06-11/police-take-taksim-square/4747650

Askari Polisi Wakipiga Risasi Za Machozi Hewani

                           kina ras makunja wa uturuki wakipereka na muziki wao hewani
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA