Meneja wa Biashara wa benki ya CRDB tawi la UDOM, Danford Muyango akitoa mada kongamano la kimataifa la vyuo vikuu vya Afrika Mashariki kuhusu ujasiriamali, ubunifu na uongozi. Vijana wasomi walikutana katika Chuo Kikuu cha Dodoma na kupata fursa ya kuelimishwa kuhusu ujasiriamali toka kwa watoa mada mbalimbali. Kongamano hilo liliandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji vya uongozi kwa vijana (AISEC) na kudhaminiwa na Benki ya CRDB.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la UDOM, Emmanuel Chaburuma akifafanua jambo kuhusu kongamano hilo.
Rais wa AISEC Tanzania, Frank Mushi
Mwanafunzi wa mwaka wa tatu UDOM, Lulu Molel akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kongamano hilo.
Baadhi ya wanafunzi wakionesha vipaji vyao
Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali wakiwa katika kongamano la kimataifa la vyuo vikuu vya Afrika Mashariki kuhusu ujasiriamali, ubunifu na uongozi. Vijana wasomi walikutana katika Chuo Kikuu cha Dodoma na kupata fursa ya kuelimishwa kuhusu ujasiriamali toka kwa watoa mada mbalimbali. Kongamano hilo liliandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji vya uongozi kwa vijana (AISEC) na kudhaminiwa na Benki ya CRDB.