MASHINDANO YA MISS WORLD KWA MWAKA 2013: WALIMBWENDE HAWATAVAA VAZI LA BIKINI . . .


Shindano la kumtafuta mrembo wa dunia kwa mwaka huu 2013 linategemewa kufanyika huko Indonesia, lakini utofauti utakaokuwepo ni kwamba washiriki hawatavaa vazi la bikini kama ilivyozoeleka katika mashindano yaliyopita.
Kwa mujibu wa mtandao wa aceshowbiz waandaaji wa shindano hilo la mrembo wa dunia 2013 wametoa taarifa ya uamuzi huo Jumanne wiki hii (June 5) ikiwa ni hatua ya kuepukana na kutofautiana na vikundi vya kiislam vya Indonesia ambayo aslilimia 90 ya wananchi wake ni waislam.
Msemaji wa RCTI waandaaji rasmi wa Miss World 2013 nchini Indonesia, Adjie S. Soeratmadjie alisema
“Kutakuwa hakuna bikini katika shindano la miss world mwaka huu ili kuheshimu mila zetu za jadi na maadili, Hili ni suala nyeti hapa Indonesia.. Tumejadiliana tangu mwaka jana na wamekubali.”
Shindano hilo linatarajiwa kufanyika mwezi september mwaka huu (2013).

news via: bongo5
Previous Post Next Post