Lil wayne ‘aitukana’ Marekani kwa namna yake!


Wa Marekani walio wengi wamesikitishwa na kitendo alichokifanya Lil Wayne baada ya kuikosea heshima nchi yao ya Marekani, kwa kuamua kuikanyaga kanyaga bendera ya nchi hiyo kwa makusudi kama vile yuko juu ya kapeti la kawaida ama tambaa la deki.
lil wayne akikanyaga bendera
Tukio hilo lilitokea wikendi hii wakati Weezy alipokuwa ana shoot video yake mpya “God Bless Amerika” huko Orleans, Marekani.
Ilianza hivi, wakati video shoot inaendelea Wayne alianza kurap mbele ya bendera kubwa ya Marekani ambayo baada ya muda ilitupwa chini na rais huyo wa Young Money hakusita kuanza kuikanyaga kwa swagg huku akiendelea kurap.
Baadhi ya mashahiri ambayo pia ni controversial ya wimbo huo yanasema “My country ’tis of thee / Sweet land of kill ‘em all and let ‘em die / God bless Amerika / This ole’ godless Amerika.”
Previous Post Next Post