Unaweza ukahisi kichwa cha habari ni kikubwa mno kuupa wimbo kama ‘Maskini Wangu’ wa marehemu Albert Mangwea uliotoka July mwaka jana. Hiyo ni kwasababu Ngwair ana hits nyingi mno ukianzia Ghetto Langu, Mikasi, aka Mimi, She got a gwan, Sikiliza, Msela, Speed 120, CNN na zingine nyingi zikiwemo alizoshirikishwa. Sio kosa lako kwakuwa ‘Maskini Wezangu’ haukupewa sana muda wa hewani na radio za Tanzania.
Sababu za kwanini haukupewa airtime inayotakiwa ni nyingi lakini kubwa ni watangazaji na madj wengi kushindwa kuiona dhahabu iliyojificha kwenye wimbo huo wenye uandishi wa kipekee kama huu. Pengine hiyo ni miongoni mwa sababu kwanini wakati mwingine Ngwair alikuwa akifedheheshwa kwa kuona wimbo kama huu unachukuliwa poa.
Mimi niliuelewa sana na ndio maana nadiriki kusema ‘Maskini Wenzangu’ ni miongoni mwa nyimbo chache za conscious Hip Hop bora kabisa kuwahi kuandikwa nchini Tanzania. Nasema kwa kujiamini kuwa Maskini Wenzangu is the best conscious hip hop song of all time.
Naweza kupata picha ya mazingira yaliyompelekea Ngwair kuandika ngoma yenye mashairi mazito kama haya. Ni aina za nyimbo ambazo msanii huandika anapokuwa katika wakati mgumu katika maisha yake na kwa kuangalia hali zilivyo ngumu kwa watu wengi wanaomzunguka.
Naufanananisha Maskini Wenzangu na wimbo wa The Game ‘One Night’ uliopo kwenye albam yake ya pili ‘Doctor’s Advocate iliyotoka n November 14, 2006 kupitia Geffen Records. Ni miongoni mwa nyimbo nyingi alizoziandika The Game alipokuwa na wakati mgumu katika maisha yake hasa baada ya kutoshwa na label ya Aftermath/G-Unit na pia kumkosa Dr. Dre kwenye projects zake.
Ukiusikiliza ‘Maskini Wenzangu’ uliotayarishwa na Manecky utagundua kwanini huwezi kumfananisha Mangwea na rapper mwingine yeyote Tanzania. Ni rappers wachache sana wenye uwezo wa kuandika nyimbo za mapenzi, party na maisha kwa uwezo sawa. Wasanii wengi wa Hip Hop huwa wazuri katika aina moja ya uandishi.
Bahati mbaya tu ni kwamba watu tunashindwa kutambua uwezo wa mtu na kuusema angali akiwa hai.
Kwenye Maskini Wenzangu Mangwea amemshirikisha mdogo wake kimuziki, Mirror ambaye hivi karibuni alichukuliwa kuwa chini ya uongozi wa kampuni ya Wema Sepetu, Endless Fame Films.
“Wachache ndo wanaishi wengi wetu ma escorts, Twiga wanapanda pipa hata bila ya passports, mikoa mingi bado haina hata airports, zaidi ya migodini madini kuya export,” anarap Ngwair.
Ni bar 4 tu lakini zenye ujumbe mzito ndani yake. Maana ni kwamba hapa nchini kuna watu wachache sana wanaoishi maisha mazuri kiasi cha kufurahia maisha huku wananchi wengi maskini wakisindikiza tu. Mbaya zaidi ni kuwa rasilimali za taifa zinawafaidisha watu wachache wenye nafasi na kuzitumia kwa matumizi yao binafsi kujilimbikizia mali.
“Viongozi wa siasa kama viongozi wa dini, mengi wanaongea coz silaha yao ni ulimi, mh.spika Tanzania huru inazidi zeeka tayari ni miaka 50, mengi mmetuahidi pia ahadi ni deni,” mistari hiyo inaakisi yale yanayoendelea sasa bungeni na jinsi ambavyo wanasiasa wameendelea kutoa ahadi zisizotekelezeka.
Website ya Leotainmenttz iliwahi kuuchambua wimbo huu kwenye ‘The Music Postmortem’ mwaka jana na wachambuzi walielezea ukubwa wa wimbo huo.
“Ubunifu alioutumia katika kuyaandika mashairi ya idea hii unaweza kuupa nafasi kubwa wimbo huu kueleweka vizuri na kuishinda ile hofu ya kwamba idea hii imezoeleka,” alisema Josefly ambaye ni mmoja wa wachambuzi wa The Postmortem na Kikaango ya jarida la Mzuka.
“Kilichonifurahisha zaidi ni jinsi mtunzi alivyojitahidi kutumia sanaa ya ubunifu karibu kwenye kila mstari ambao ungeweza kuwa wa kawaida tu kama angeusema vile vile bila kutumia huu ubunifu. Mfano, ‘..Ndo maana wazanzibar wamechoka kutanga na nyika” hapo ujumbe kuhusu muungano..neno kutanga-na nyika limetumiwa vizuri sana kuleta picha ya tatizo la muungano,…na maneno “big up Mandela leo South sio Africa” utaona neno South Africa lilivyotumika kusifia maendeleo ya South Africa,” aliendelea.
“Utunzi wa mtindo huu wa kucheza na maneno kama nilivyosema hapo juu unafanya verse ya kwanza kuwa fupi sana kwa kusikiliza. Pia mtunzi amefaulu kwa kiasi kikubwa kumfanya msikilizaji wa wimbo huu kuendelea kusikiliza zaidi kwa jinsi alivyoweza kupangilia na kumaliza na kitu kinachokuacha utafakari huku unasubiri ubeti wa pili… “leta mgomo baridi uijue serikali then muulize ULIMBOKA umuhimu wa madaktari. Hapa wengi watatafakari kwa sababu Ulimboka na swala la madaktari ni kitu ambacho kilileka attention ya wengi Tanzania.
Hata katika ubeti wa pili na wa tatu ameendelea kucheza tu na maneno huku ujumbe ukiwa ni wa moja kwa moja (direct), mfano “tunaishi kiMungu-Mungu, toa M uweke Z upate kiZunguZungu”. Hapa msikilizaji pia atatafakari, na hapa atakua ameshirikishwa kuutafakari wimbo, akitoa M kwenye neno kiMunguMungu na akaweka Z.
Naweza kusema kuwa huu mtindo alioutumia katika utunzi ndio umeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa sana kufikisha ujumbe wa moja kwa moja na unaweza kuuongezea muda wa kuishi katika masikio ya wasikilizaji, ukizingatia matukio aliyoyaweka ambayo mengi ni ya hivi karibuni. Tone aliyoitumia ni ya kulalamika ambayo inaendana kabisa na idea ya wimbo, ‘Nalia na masikini wenzangu’. Mdundo(beat) ni mzuri sana kwa jinsi ulivyofiti kwenye wimbo, kazi nzuri AM records.”
“Binafsi nilimmiss Ngwair, “alisema mchambuzi mwingine aitwaye Kinye ambaye ni Tutorial Assistant kwenye chuo kikuu cha St. Augustine University, mtunzi wa nyimbo, producer na muimbaji.
“Siku zote nimekuwa nikimpenda yeye wa namna hii…nikimaanisha yeye wa kuimba nyimbo zilizo serious sana “ni kwasababu tu kuwa anaziweza sana”…kwa waliopata bahati ya kuisikiliza a.k.a mimi watakuwa wanaungana name kuguswa na nyimbo kama sikiliza, zawadi, na a.k.a mimi ukiicha pembeni Jah Kaya ambayo ilitugawa mashabiki wake “si sana”
“Maskini Wenzangu”…title nzuri ambayo inamshawishi kila mmoja kutamani kusikia kilichoimbwa ndani. Hakika kila kilichoibwa ndani kimenifanya nilibariki jina la wimbo huu na si kufanya ubatizo wa jina jipya,”alimalizia Kinye.
Pata muda wa kuusikiliza wimbo huu na kusoma mashairi yake hapo chini huenda ukakubaliana name. RIP Albert Mangwea, you will be missed.

Mirro akiwa na Wema Sepetu
Katika Maskini Wenzangu, Ngwair amevaa viatu vya Watanzania wengi wanaoishi maishi ya umaskini mkubwa unaochangiwa na uongozi mbaya wa serikali unaoruhusu kuwepo nafasi ya watu wachache kula karibu asilimia 85 ya keki ya taifa.