FACEBOOK WAZINDUA KITU KIPYA 'VERIFIED ACCOUNTS' YA KUTAMBUA AKAUNTI HALISI ZA MASTAA





Mtandao maarufu wa kijamii wa Facebook umeanzisha ‘verified pages/accounts’ kwa lengo la kuwasaidia watu mbalimbali kuzitambua akaunti halisi za watu maarufu na wenye high profile walioko katika mtandao huo.



Kwa Mujibu wa mtandao wa Digital spy, Facebook wamesema wanahitaji kusaidia watu kuzitambua akaunti halisi za macelebrity au watu wenge high profile katika jamii pamoja na biashara zenye majina makubwa, na kuongeza kuwa hii itakuwa ni kwa kundi dogo la watu mashuhuri.

Ili kuitambua ‘kurasa halisi (verified pages) ktika mtandao wa Facebook, itakuwa na alama ndogo ya tiki ya rangi ya blue kama verification ya watu maarufu katika jamii wakiwemo celebrities, viongozi wa serikali, waandishi wa habari maarufu, bila kusahahu makampuni au bidhaa maarufu, hivyo itakuwa rahisi kwa mtu kuweza kufahamu kama page ambayo amelike ama akaunti ambayo ame subscribe ni halisi au fake.



Tiki inayotambulisha verified page/account iliyoongezwa na Facebook inafanana na ile ya verified accounts za Twitter.

Ili mtu maarufu kuweza kupata ‘verified account’ katika mtandao wa Facebook, mhusika atahitajika kuwasilisha kitambulisho halali kinachotambuliwa kiserikali ikiwa ni moja ya hatua za kuwa verified.

Hii ni habari njema sana kwa mastaa wote duniani (hasa Tanzania) ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipata shida kutokana na watu wengine kufungua akaunti za uongo katika Facebook zikionesha kuwa ni zao na hivyo kuwachanganya watu wanaodhania kuwa ni zao.
Previous Post Next Post