Beyonce atumia mapumziko ya Mrs. Carter World Tour kwa ajili ya familia na Mtoto wake Kipenzi Blue Ivy na Kumpeleka kwenye michezo ya watoto




Pamoja na ratiba ngumu za ubusy wa wazazi wake ambao muda mwingi huwa wako katika tour, mtoto Blue Ivy bado anapata haki zake za msingi kutoka kwa wazazi wake, ambapo weekend iliyopita Beyonce ameonekana na mwanae wakifurahi katika park yenye michezo mbalimbali huko New York , Marekani.


Beyonce ameitumia weekend hii kufanya mambo mengi ya kifamilia, ikiwa ni pamoja na kuungana na mumewe kumsupport swahiba wao Kanye West katika sherehe yake ya kuzaliwa, na kisha alitenga muda wa kufanya shopping na kumpeleka mwanae Blue Ivy katika viwanja vya michezo na kufurahi naye.


Upande mwingine Mrs. Carter ambaye mara kadhaa hupenda kuandika ujumbe kwa mkono wake mwenyewe kwa watu anaowapenda, alimwandikia ujumbe wa pongezi mcheza tennis maarufu Serena Williams kutokana na ushindi wa French Open alioupata hivi karibuni. Mtu mwingine ambaye Bey amewahi kumwandikia ujumbe kwa mkono ni pamoja na mke wa rais wa Marekani Michelle Obama.


Kwa sasa Beyonce yuko katika mapumziko mafupi ya Mrs. Carter World Tour.
Previous Post Next Post

Popular Items