MAZOEZI kwa ajili ya kujiandaa na shindano la kumsaka malkia wa Mkoa wa Tanga mwaka huu "Redd's Miss Tanga 2013" yanatarajia kuanza Jumatano Mei 8 kwenye Ukumbi wa Lavida uliopo jijini Tanga.
Akizungumza na Ripota wa Globu ya Jamii, Mkurugezi wa Kampuni ya DATK Intertaimeint, Asha Kigundula ambae ndie Mratibu wa shindano hilo, alisema kuwa maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vizuri. Kigundula alisema kuwa walimu watakaosimamia warembo hao ni Miis Tanga 2012 Teresia Kimolo na Miss Tanga 2011 Zubeda Seif.
Alisema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri, ambapo warembo wameanza kuitikia wito wa kushirikishi shindano hilo. Kigundula alisema kuwa mpaka sasa jumla ya warembo 8 wamejitokeza kushiriki shindano hilo ambapo nafasi bado iko wazi kwa wasichana wote wenye sifa za kushiriki.
"Kila kitu kinaendelea vizuri, ikiwa na warembo kuendelea kujiandikisha kushiriki shindano la mwaka huu, ambalo nina hakika litakuwa la aina yake"alisema Kigundula Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo mkoani humo kwa kuwa Kampuni DATK imejipanga, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wa jijini hapo kwa ujumla wakae mkao wa kupata raha.
Pia alisema fomu zinapatika katika ofisi ya Mwananchi iliyopo Bandari Tanga ghorofa ya Nne, Five Brathers kwa Nassa Makau iliyopo jijini humo, kwa Dar es Salaam zinapatikana katika ofisi za Jambo Leo zilizopo Jengo la Hifadhi Hause Posta.