BREAKING NEWS: MITIHANI KIDATO CHA NNE KUSAHIHISHWA UPYA




Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyeunda tume ya kuchunguza kufeli kwa wanafunzi wengi mwaka 2012.

………………………………………………………..

Tume ilioundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuchunguza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana, LEO imeitaka serikali ifute matokeo yote na mitihani isahihishwe upya.

Akisoma ripoti ya Tume hiyo hivi punde bungeni Mjini Dodoma, Waziri wa Nchi Katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia sera na uratibu, William Lukuvi amesema kwamba mitihani hiyo inapaswa kusahihishiwa kwa kuzingatia vigezo vilivyotumika katika kusahihisha mitihani ya kidato cha nne mwaka 2011.

Mwaka jana matokeo ya wanafunzi wa kidato cha nne yalikuwa mabaya kuliko matokeo mengine yaliowahi kutolewa na Baraza la Mitihani la Taifa. Wanafunzi walifeli kwa asililimia 60.

Kutokana na matokeo ya tume hiyo, Lukuvi ameipongeza tume hiyo kwa kutoa matokeo hayo.

Wataalamu wa elimu wanasema kwamba endapo serikali itatekeleza pendekezo hilo itaingia kwenye gharama kubwa ambazo pengine zitaigharimu serikali.
Previous Post Next Post