Video: Nicki Minaj ‘amsurprise’ Lil Wayne kwenye Billboard Music Awards 2013 kwa kumchezea kimahaba jukwaani





Onika Tanya Maraj anayefahamika zaidi kama Nicki Minaj ni moja ya wasanii walio perform jana (May 19) kwenye show ya Billboard Music Awards 2013 huko Las Vegas, Marekani. Wakati yuko jukwaani akimalizia kuimba hit song yake ya ‘High School’ aliamua kuongeza manjonjo ambayo watu hawakutegemea.
lil wayne n nicki
Kama zilivyo events nyingi zinazowahusisha wanamuziki maarufu, huwa hapakosi matukio ya tofauti ya kujadiliwa zaidi baada ya show kuisha. Wakati Minaj akimalizia kuperform wimbo wa ‘High School’alimvamia boss wake wa Young Money, Lil Wayne ambaye amemshirikisha katika wimbo huo, na kumfanyia ‘lapdance’ mtindo ambao huwa unatumika na strippers katika strip dance kwa lengo la kuvuta hisia fulani za kimahaba.
Minaj alimfuata Weezy aliyekuwa amekaa kwenye kiti hapo jukwaani na kumkatikia juu yake lakini ile kimahaba zaidi na kumfanya Lil wayne kushika kichwa kuonesha hakutegemea.
Rapper Nicki Minaj mwenye miaka 30 alifanikiwa kuondoka na tuzo 3 hiyo jana ambazo ni Top Streaming Artist, Top Rap Artist and Top Rap Album (“Pink Friday: Roman Reloaded”).
Tazama video hiyo hapa:

Previous Post Next Post