ULE UFUNGUZI WA FLAGSHIP STORE YA SHERIA NGOWI UKO HAPA [PICHA]



Mbunifu wa mavazi nchini, Sheria Ngowi, leo amefungua duka lake maalum la nguo ‘flagshop store’ lililopo maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam. Tofauti na maduka mengi ya nguo yaliyozoeleka, wateja watakuwa wakienda kupitia appointment maalum.


Uzinduzi huo umehudhuriwa na watu mbalimbali mashuhuri akiwemo naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, Meya wa Ilala Jerry Slaa pamoja na Mwamvita Makamba ambaye ni mwekezaji kwenye brand ya Sheria Ngowi. Wengine ni mamiss Tanzania wa zamani, Faraja Kotta na Nancy Sumari, Miss universe wa zamani Flaviana Matata, Mwana FA na wengine.



Akiongea na Bongo5 mara baada ya duka lake kufunguliwa rasmi, Sheria Ngowi amesema siku hii imekuwa ni muhimu kwake na amekuwa na furaha kubwa kufanikisha hatua hiyo.

“Ni kitu ambacho nilikiwa nimekiplan muda mrefu sana na in the end unaona kitu kama hiki sasa hivi. Kwangu mimi sio kwamba ni mafanikio makubwa sana ila ni mwanzo wa mafanikio kwahiyo bado nina kazi, sababu leo tumefurahia kesho nataka tufurahie zaidi, leo tupo Masaki kesho tupo New York,” amesema Sheria.

Duka hilo lipo Masaki, mtaa wa Buzwagi.
























































NEWS AND PICS FROM BONGO5.COM
Previous Post Next Post