Wiki hii mwimbaji wa RnB ambaye pia ni kaka mwanadada Brandy Norwood, Ray J alikuwa mgeni katika TV show maarufu ya 106 & Park ya BET akiwa na company ya mrembo aliyeonekana katika video ya wimbo wake wenye utata “I hit it first”.
![](http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2013/05/Ray-J-kim-21.jpg)
Mrembo huyo aitwaye Luba mwenye muonekano kuanzia sura, urefu, smile kama ya ex girlfriend wa Ray J, Kim Kardashian aliongozana na Ray J kwa lengo la kutambulishwa kama mrembo aliyecheza kwenye video hiyo na pia Ray J aKielezea mambo mengi kuhusiana na single hiyo iliyomake headlines baada ya kutoka kutokana na kuwa controversial.
![](http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2013/05/kim-Luna.jpg)
Show ya 106 & Park inaongozwa na watangazaji wanne wakiwemo rapper Shad “Bow Wow” Moss, Jordan “Shorty da Prince” Johnson, na warembo Kimberly “Paigion” Walker na Mykel “Miss Mykie” Gray
![](http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2013/05/ray-106-2.jpg)