CRIS BROWN AANZISHA CHANNEL ITAYOMWEZESHA KUWASILIANA NA FANS WAKE KWA UKARIBU ZAIDI NA KUONUESHA MAISHA YAKE MUDA NA WAKATI WOWOTE






Mashabiki wa muimbaji wa ‘Fine China’ Chris Brown sasa wanaweza kujionea mambo mengi yanayoendelea katika maisha yake baada ya kuanzisha mtandao wake ‘Chris Brown Channel’ utakaokua ukionesha maisha yake 24/7.


Chris Brown Channel ni zaidi ya akaunti zake za twitter, facebook, Instagram na hata youtube sababu mashabiki wake watakua na nafasi kufahamu na kujionea mengi yanayoendelea katika maisha ya superstar huyo kwa saa zote 24 katika siku 7.



Katika mtandao huo, CB atakuwa akiweka updates za kazi zake, na maisha yake ya kawaida, picha pamoja na video za sehemu anazokuwepo kama akiwa anacheza Basketball, akiwa backstage wakati wa show zake, anapokuwa akichill na washikaji zake, na je akiwa ana hookup na wapenzi wake?? Ngoja tutaona.

Kwa mara ya kwanza Chris amepost broadcast yake ya kwanza kupitia channel hiyo Jumatano (May 15) akiwakaribisha watu katika channel yake mpya, “sasa mnaweza kuniona muda wote katika siku na kujua kila ninachokifanya, nawashukuru sana na ninawapenda,” alisema Chris katika video clip yenye urefu wa sekunde 13.
Previous Post Next Post

Popular Items