Mtanzania ambaye kwa sasa ni raia wa Uingereza na anayechezea klabu ya Chelsea, Adam Nditi ameiponda show ya Diamond mjini Reading nchini humo na kudai ilikuwa ni aibu tupu.

“Diamond jana manyago aibu tupu waswahili lazima tubadilike it’s embarrassing,” ametweet.
“Hajafanya jambo lolote ila shoo ilikuwa haina very unprofessional kwenye tangazo walisema inaanza saa 3 usiku jamaa amefika saa 1 asubuhi.”
“Jukwaa lilikuwa ovyo kama vile watu hawajalipa kumuuona mmoja Wa wasani wanaotamba bongo nyimbo zilikuwa zinapigwa redioni alikuwa haimbi.”
Diamond yupo ziarani nchini Uingereza.