50 CENT AJITOLEA KUGHARAMIKIA MAZISHI YA MTOTO WA KIKE WA MIAKA 14 ALIYEPIGWA RISASI



Curtis Jackson a.k.a 50 Cent ameamua kufanya kitu kwaajili ya jamii kwa kujitolea kugharamikia mazishi ya mtoto wa kike mwenye miaka 14 aliyeuwawa kwa kupigwa risasi.


Weekend iliyopita rapper huyo alitoa pesa katika mfuko wake kwaajili ya familia ya mtoto huyo aitwaye D’aja Robinson aliyeuawa njiani akitokea katika party a sweet 16 huko Queens baada ya kupigwa risasi akiwa kwenye basi.

Tukio hilo liliwagusa wengi akiwemo Curtis ambaye aliamua kwenda hadi kwa wazazi wa mtoto huyo na kujitolea kugharamia shughuli zote na kuhudhuria mazishi.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook Curtis aliandika “Watu huwa wananipakazia picha mbaya kuhusu mimi, lakini mimi ni mtu wa kweli hapa duniani na sijasahau nilipotoka. Nimekuja kumsaidia huduma za mazishi ya huyu mtoto wa kike. Alikuwa mzuri, innocent na hakustahili kifo cha namna ile R.I.P D’Asia Robinson”

Kwa mujibu wa mtandao wa New York post, mtoto huyo alipigwa risasi kwa bahati mbaya sababu hakuwa mlengwa wa shambulio hilo.
Previous Post Next Post