RICK ROSS AINGIA MATATANI KWA MASHAIRI YA UBAKAJI



Kutokana na kuimba mashairi kuhusu kumuwekea kidonge cha madawa ya kulevya mwanamke katika kinywaji chake na kumchukua kwenda naye nyumbani Rapa Rick Rose amekalia kuti kavu kutokana na kitendo hiko

Bosi huyo wa lebo ya kurekodi muziki ya Maybach Music amejibu shtuma dhidi yake akisema hakueleweka

"Natia kidonge kwenye shampeni yake wala hakujua namchukua kwenda naye nyumbani na nikafurahia wala hakujua" alirap muimbaji huo katika nyimbo hiyo ambapo ameiweka katika albamu ya nyimbo mchanganyiko ya 'Gift of Gab 2

Wakati alipotembelea kituo cha radio cha Q93 cha mjini New Orleans wiki hii Rozay alikanusha kwamba mashairi hayo yanamaanisha kubaka

"Nataka kuliweka wazi hili kuwa mwanamke ni zawadi bora zaidi inayofahamika kwa mwanaume" aliongezea kuwa " kumetokea kwa kutoeleweka kwa mashairi na hakuna neno lililotajwa kubaka

Pia alijiweka mbali na tuhuma "lakini kamwe siwezi kulitumia neno kubaka katika mashaili yangu pamoja na kambi yangu
Previous Post Next Post