Kutokana na umamuzi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kupandisha nauli za usafiri wa mabasi,treni na gharama za bandari zitakazoanza kutumika April 12 mwaka huu, usafiri wa daladala jijini umeanza kuonekana wa shida, hasa nyakati za jioni ,kwani baadhi ya wenye mabasi ya daladala jijini Dar es Salaam wameanza kutumia mwanya huo na kuongeza nauli kinyemela hivyo kusababisha wananchi kutaabika na kusongama katika vituo vya usafiri kama wanavyoonekana baadhi yawananchi katika maeneo mbalimbali jijini ambapo wakisubiri daladala na wengine wakiamua kutembea kwa miguu.
Baadhi ya wanachi katika maeneo ya Jangwani jana wakitembea kwa miguu.baada ya kuona tatizo la kususbiri usafiri .
Baadhi ya wakazi wa jijni wakisubiri usafiri jana katika maeneo ya kituo cha Akiba mtaa wa Bibi Titi.
Baadhi ya wakazi jijini Dar es Salaam jana wakisubiri usafiri katika maeneo ya shule ya Sekondari ya Azania.