Askari wa Jeshi la wananchi wakiwa katika operesheni ya kuokoa majeruhi na kutafuta miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo huko Moshono mkoani Arusha (Picha kwa hisani ya Mtandao wa Grobalpublishers).
……………………………………………………………..
Na Gladness Mushi wa Fullshangwe-Arusha
Zaidi ya wachimbaji 25 wa moramu wanasadikiwa kufa huku watu zaidi ya sasa 14 wakiwa wamepoteza maisha kutokana na kuagukiwa na kifusi” wakati wakiwa kwenye shuguli zao za uchimbaji mawe ya moramu katika eneo la Moshono jijini
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa lilitokea asubuhi ya leo kati ya saa nne na saa tano za asubui ambapo vijana hao walishuka katika mgodi huo kwa malengo ya kuchimba Moramu
Tukio hilo lilitokea kati ya saa nne na saa tano za asubuhi mara baada ya mgodi huo kujaa maji kutokana na mvua kubwa ambazo zinanyesha mkoani Arusha hali ambayo ilisababisha mawe ya migodini kushuka ndani ya mgodi huo ukiwa na wachimbaji pamoja na madereva wa magari ya kubebea moramu hizo
Mvua kubwa ikiwa inaendelea kunyesha baadhi ya watu waliokuwa juu ya mgodi huo waliona kimya kimezidi kwa muda mrefu sana kwa kuwa sio kawaida ya wachimbaji wa mgodi huo kukaa muda mrefu bila shughuli zozote kuendelea mgondini hapo.
Ilibidi wasogee katika mgodi huo ambapo giza kubwa ambalo liliwatatanisha sana hali ambayo iliwafanya wapigiane simu na kukusanyika katika eneo hilo ambapo walianza uchunguzi na kugundua kuwa kifusi kubwa sana kilikuwa kimeshkuka katika mgodi huo na kufukia wachuimbaji hao.