Watazamaji 7,412 wameshuhudia pambano la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Toto Africans lililochezwa jana (Machi 9 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuingiza sh. 42,508,000. Mechi hiyo namba 135
iliyochezeshwa na Andrew Shamba kutoka mkoani Pwani ilimalizika kwa Yanga ambao wanaongoza VPL wakiwa na pointi 45 kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 9,406,764.95 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 6,484,271.19.
Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 6,708 na kuingiza sh. 33,540,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 89 na kuingiza sh. 1,780,000.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 4,783,100.82, tiketi sh. 4,136,390, gharama za mechi sh. 2,869,860.49, Kamati ya Ligi sh. 2,869,860.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,434,930.25 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,116,056.86.
Tags:
Sports