MAONYESHO YA ITB MJINI BERLIN


1Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dk. Aloyce Nzuki akiwa katika mazungumzo na Rica Rwigamba Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Rwanda wakati alipokutana katika maonyesho ya dunia ya Utalii ITB yanayofanyika kwenye jengo la Messe Berlin jijini Berlin Ujerumani, Monyesho hayo yanahusisha makampuni yenye kutoa huduma mbalimbali za utalii duniani ambao hukutana na kutangaza utalii wa nchi zao huku wakifanya makubaliano  na kuingia  mikataba mbalimbali ya  kuuziana bidhaa za kitalii, Maonyesho hayo yanamalizika rasmi leo. 2Mkurugenzi wa Kampuni ya ndege ya Flightlink  Capt. Munawer Dhirani akizungumza na Ibrahim Mussa Mkurgenzi wa Utalii Wizara ya Maliasili na Utalii  katikati ni Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Christopher Mvula  akisikiliza kwa makini wakati Balozi huyo alipotembelea katika banda la Tanzania kwenye maonyesho ya ITB yanayomalizika leo jijini Berlin Ujerumani kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dk. Aloyce Nzuki 
4
Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Geofrey Meena kushoto akitembelea Banda la Kampuni ya Pongo Safaris katika maonyesho ya Utalii ya ITB,  wengine  kutoka kulia ni Marlon Van Hee Meneja Mradi wa kampuni ya ECEAT PROJECTS ya Uholanzi ,Julias Alexander Pundo Mwakilishi wa kampuni ya Ramogi Tours & Travel Limited Jumuiya ya Ulaya na Cynthia Ponera Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Pongo Safaris 6 
Wadau wa Ujerumani hawakukosa kutembelea maonyesho hayo hapa walikuwa wakipata Menyu wakati wa hafla ya Jumuiya ya Afrika Mashariki 10
Team Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kazi kubwa ya kuuza utalii wa Tanzania kwenye maonyesho hayo. 11
Hapa ni kwenye Banda la Pongo Safaris na Ramogi Tours  pichani ni Julius wa Ramogi Tours pamoja na Cynthia wa Pongo Safaris 12
  Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Christopher Mvula akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya ndege ya Flightlink  Capt. Munawer Dhirani  wakati walipokutana katika maonyesho hayo
9
Huu nao ulikuwa ni utalii wa aina yake katika maonyesho hayo ambapo watu mbalimbali walikuwa wakipiga nao picha kwa ajili ya kumbukumbu zao
Previous Post Next Post