Mkuu wa Wilaya ya Mfia Sauda Mtondoo akimkabidhi Prudence Nyombi zawadi ya King’amuzi cha Star timu baada ya kujishindia kutokana na kujibu swali aliloulizwa juu ya matumizi ya Mawasiliano, wakati wa Semina ya Majukumu ya Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Mashariki iliyofanyika Wilayani Mafia.katikati ni Mkurugenzi wa Watumiaji na Watoa Huduma za Mawasiliano Dk. Raymond Mfungahema akishuhudia.
Mhasibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Kanda ya Mashariki Patrice Lumumba akitoa maada ya Mfumo wa Anuani za Makazi na Posti Kodi wakati wa Semina ya Majukumu ya Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Mashariki iliyofanyika Wilayani Mafia.
……………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Mawasiliano nchini, kanda ya mashariki imetoa rai kwa watumiaji wa mitandao ya simu za mkononi kuwa macho na wizi unaofanywa na watu wenye nia ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, ambapo idadi kubwa ya wateja wa simu wamejikuta wakilalamikia wizi huo.
Mojawapo mwa udanganyifu ni pamoja na mmiliki wa simu kutumiwa ujumbe unahitaji kutuma fedha kwa ajili ya kulipia gharama za huduma kwa njia mtandao ili hali anayetumiwa fedha hizo hafahamiki.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Watumiaji na watoa huduma za Mawasiliano Dk. Raymond Mfungahema wakati alipokuwa akitoa mada ya kazi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Mfia waliohudhuria katika Semina ya Majukumu ya Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Masharaiki
Afisa Utumishi Mkuu,Esuvatie Masinga katika Semina ya Majukumu ya Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Mashariki, iliyofanyika kisiwani Mafia.
Semina hiyo iliyofanyika Machi 7 mwaka huu iliwashirikisha wadau mbalimbalimbali wa mawasiliano wilayani Mafia, wakiwemo watendaji wa serikali wa ngazi ya kitongoji, kata na tarafa na wilaya.
Katika semina hiyo iliyohudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya Mafia, Sauda Mtondoo ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi,Masinga alisema, wizi wa mitandao ya simu ni changamoto iliyo mbele ya wateja ambayo inaweza ikakabiliwa kama kila mmoja atakuwa na ufahamu wa kubaini ujanja na mbinu zinazofanywa na wajanja wachache.
Alisema ili kukabiliana na mbinu na ujanja wa wachache hao, wamiliki wa simu za mkononi wanatakiwa kuwa macho ujumbe wowote unaozungumzia utumaji wa fedha iwe kwa njia ya ujumbe mfupi ama mawasiliano ya moja kwa ya simu wa watu wasiowajua.
Amesema,wateja wengi wamekuwa wakitumiwa ujumbe unaowataka watume fedha kwa watu wasiowajuwa wakiamini kuwa wanatuma fedha hizo kwa makampuni ya simu, jambo ambalo si kweli, kwani makampuni yote ya simu yana namba zao za utambulisho pindi wanapoendesha zoezi lolote la kihalali.
Tags:
Technology