WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Mwananchi Communications, wametembea katikati ya moto unaowaka.
Wafanyakazi hao wameweka kambi ya siku tatu katika Hoteli ya kitalii ya Beach Comber, iliyopo katika fukwe
za bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam, zoezi hilo la kutembea kwenye moto ni sehemu ya utekelezezaji wa
majukumu ya Kampuni hiyo yenye lengo la kuinua viwango vya wafanyakazi wake na kuwapa ujasili wa kufanya
maamuuzi magumu,katika utendaji wao kazi.