MAKADINALI VATICAN WAANZA MAANDALIZI YA KUMCHAGUA PAPA MPYA


Maandalizi ya kuanza kwa mchakato wa uchaguzi wa papa mpya yameanza leo mjini Vatican, ambapo baraza la Makadinali limefungua mazunguzo ya kila siku kujadili sifa za papa ajaye na kutafakari nani miongoni mwao anaweza kufaa kwa nafasi hiyo.
Nia kuhakikisha papa anachaguliwa katika wiki ijayo na kumsimika rasmi siku kadhaa baadaye, ili aweze kuhudhuria sherehe za wiki takatifu, kuanzia Jumapili ya Matawi tarehe 24 Machi, na Pasaka katika Jumapili itakayofuatia.
Viongozi hao wanatarajiwa kufanya mikutano ya asubuhi na mchana katika jitihada za kujadili kadiri iwezekanavyo katika kipindi kifupi.
Orodha ya changamoto zinazolikabili kanisa hilo linalokabiliwa na migogoro inaweza kuchukua wiki kadhaa kujadiliwa, lakini Vatican imeonyesha nia ya kumaliza mazungumzo hayo ndani ya wiki moja ili Makadinali 115 wanaopaswa kupiga kura watekeleze jukumu lao.

Previous Post Next Post