HVI NDIVYO JINSI WAFANYAKAZI WA GAZETI LA MWANANCHI WALIVYOTEMBEA NDANI YA MOTO


WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Mwananchi Communications, wametembea katikati ya moto unaowaka.
Wafanyakazi hao wameweka kambi ya siku tatu katika Hoteli ya kitalii ya Beach Comber, iliyopo katika fukwe
za bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam, zoezi hilo la kutembea kwenye moto ni sehemu ya utekelezezaji wa 
majukumu ya Kampuni hiyo yenye lengo la kuinua viwango vya wafanyakazi wake na kuwapa ujasili wa kufanya
maamuuzi magumu,katika utendaji wao kazi pamoja na kujiletea maendeleo katika maisha yao ndani na nje ya
Kampuni hiyo.
Ilikutizama picha zingine za tukio hilo bovya maandishi ya blue 

Wafanyakazi wa Gazeti la Mwananchi watembea kwenye moto


Anne kutoka idara ya matangazo Mkoa wa Mbeya pia alionyesha ujasiri wake na kupita ndani ya moto huo
Hii ndiyo moja ya mbinu ya mafanikio katika maisha ya binadamu, kwani mafanikio yanahitaji ujasiri hasa wakati wa kufanya maamuzi magumu katika maendeleo
Kwa kawaida zoezi la kupita ndani ya moto unaowaka ni jambo gumu sana,lakini katika suala la malengo na ufanisi kazini na maendeleo ya maisha ya bindamu ni jambo rahisi sana kwani utapita ndani ya moto huo bila kuungua
Kushoto ni Mwandishi wa Gazeti la Mwanaspoti Doris Mariaga na mfanyakazi mwenzake akitimiza lengo la ufanisi kazini
Ujasili na ukakamavu ndiyo dawa pekee iliyotakiwa katika zoezi hilo
Wengine walikimbia huku wengine wakitembea kwa madaha
Kila mfanyakazi alifanikiwa kupita ndani ya moto huo kwa staili ya aina yake
Kulia ni mhariri wa Gazeti la The Citizen Kimolo na Sele kutoka Kiwandani wakipita ndani ya moto huo
Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Mkoa wa Mbeya, Brand Nelson (a.k.a Ninja) kulia akipita ndani ya moto unaowaka kushuto ni Mwandishi wa The East Africa Rosemary Mirondo akikwepa moto huo.
Kulia ni Deo kutoka Mwanza akupita ndani ya moto

Read 161 times

Previous Post Next Post