TBL YATOA MSAADA WA MAGODORO 210, VYANDARUA 200 HOSPITALI MKOANI KILIMANJARO


 
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (katikati), akimkabidhi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Ibrahim Msengi  msaada wa magodoro kwa ajili ya Hosptali ya Huruma ya wilayani Rombo pamoja na Kituo cha Afya cha Uru Kiaseni katika hafla iliyofanyika Mjini Moshi. Kulia kwake ni Mganga Mkuu wa mkoa huo, Dk. Mtumwa Mwako. Jumla ya magodoro 210 na vyandarua 200 vimetolewa na TBL kwa ajili ya kituo hicho na hospitali hiyo.
 
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Ibrahim Msengi akikabidhi msaada wa magodoro kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Mtumwa Mwako baada ya kukabidhiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), mjini Moshi . Katikati ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo. Jumla ya magodoro 210 na vyandarua 200 vimlitolewa na TBL kwa ajili ya kituo Afya cha Uru Kiaseni na Hosptali ya Uhuruma .

 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL, Steve Kilindo,(katikati)wakifurahia jambo na kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dk Ibrahm Msengi (Kulia )pamoja na mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dk Mtumwa Mwako mara baada yaTBL  kukabidhi msaada wa magodoro 210 na vyandarua 200 kwa kituo cha Afya cha Uru Kiaseni na hosptali ya Uhuruma .
 
 
Mganga wa kituo cha Afya cha Rau Kiaseni  Dk. Delfina Materu(katikati)akizungumza na wanahabari (hawako pichani)mara baada ya kupokea msaada wa Magodoro kutoka kampuni ya bia Tanzania(TBL)shoto kwake ni Meneja mauzo wa TBL mkoa wa Kilimanjaro Leiya Hermenegild.
WADHAMINI wakuu wa mbio za Kilimanjaro Marathon, kampuni ya Bia ya TBL, imekabidhi  msaada wa magodoro na vyandarua kwa uongozi wa hosptali ya Huruma na kituo cha Afya cha Uru Kiaseni kama  sehemu yamaandalizi ya mbio za Kilimanjaro marathon zinatarajia kufanyika leo machi 3.
Misaada ya aina hiyo hufanywa kila mwaka na TBL wakati wa  maandalizi ya Mbio za Kilimanjaro Marathon ambazo hufanyika kila mwaka ikiwa ni utaratibu wa kampuni hiyo kurudisha faida iliyopatikana kwa wananchi kutokana na utumiaji wa bidhaa zake.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano, Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo, alisema kuwa TBL imeamua kufanyautaratibu huo ambao wamekuwa wakifanya kila mwaka na mwaka huu wameonelea ni vyema wakatoa msaada katika hospitali hizo.
Kilindo alisema kuwa msaada wa magodoro hayo 210 na vyandarua 200 ni jitihada za kampuni hiyo kuhakikisa jamii  ya Tanzania inafurahi na kujivunia kilicho chao na kuongeza kuwa hicho wal;ichokitoa ni sehemu ya shukuruni kwa watanzania ambao wamekuwa wakiwaunga mkono kila mara.
“Kama wadhamini wakuu wa mbio hizi, tumekuwa tukishiriki katika shughuli nyingi za kijamii na moja yao ni kutoa msaada katika mahospitali, leo tunatoa magodoro 210 na vyandarua 200 kwa hospitali za Kiaseni ya Rau na Huruma ya Rombo, tunaamini katika hili tutakuwa tuimesaidia kwa kiasi fulani,” alisema Kilindi Naye Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Ibrahimu Msengi akipokea msaada huo kwa niaba ya uongozi wa hospitali hizo aliipongeza TBL kwa kuamua kuijali jamii inayonunua na kutumia bidhaa zao na kuongeza kuwa msaada huo anaamini utakuwa wa manufaa makubwa kwa wagonjwa katika hospitali hizo.
“Moyo wa kutoa sio lazima uwe nacho, TBL wameonesha kuwa kazi yao sio kutengeneza bia tu, bali wanaweza kujali jamii na katika hili nawapongeza sana na ningependa mashirika na makampuni mengine nayoyangekuwa yanafanya hivi,” alisema Msengi.
Msengi alitoa wito kwa wafanyabiashara wote na wamiliki wa makampuni kuiga mfano mzuri ulioonesha na TBl na kusisitiza umuhimu wa kutoa kwani jukumu la kuhudumia jamii ni la kila mtu na sio serikali pekee.
Kuhusu mbio za mwaka huu za Kilimanjaro marathon Dkt. Msengi alisema,mbio hizo kufanyika katika ardhi ya Kilimanjaro ni fahari na kuongeza kuwa matarajio ya wote ni kuona kila mtu akinufaika na mbio hizo huku akiwatakia kila kheri wakimbiaji wote hasa wakimbiaji wa Tanzania.
“Nitumie Fursa hii kuwatakia kila la Kheri wakimbiaji wote wa Kilimanjaro marathon, kila la kheri watanzania wote watakaotuwakilisha keshokutwa naamini tutashinda,” alisema.
Kwa upande wake Mganga mnku wa mkoa wa Kilimanjaro (RMO), Dk. Mtumwa Mwako, akipokea magodoro na vyandarua hivyo kutoka kwa kaimu mkuu wa mkoa kwa niaba ya uongozi wa Hospitali za Kiaseni na Huruma, alisema kuwa msaada huo utasaidia kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Malaria kwa mama na mtoto.
Nao madaktari kutoka katika hospitali hizo, Dkt. Godwin Kiwelu wa hospitali ya Huruma ya Rombo na Dk. Delfina Materu wa hospitali ya Kiaseni ya Rau, walisema kwa msaada huo mzigo wa changamoto zinazokabili hospitali hizo zimepungua huku wakisisitiza kuwa bado kuna changamoto nyngi ambazo inatakiwa jamii inatakiwa kujitokeza kusaidia kama walivyofanya TBL.

Previous Post Next Post

Popular Items