ST. ANTONY MBAGALA YAPOKEA VIFAA VYA MUZIKI KUTOKA KAMPUNI YA PONGO SAFARIS


1
Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Pongo Safaris Bi Scholastica Ponera akikabidhi vifaa vya ngoma za asili kwa Ismail Edward Mkuu wa shule ya Sekondari ya St. Antony Mbagala jijini Dar es salaam hivi karibuni, huo ni msaada aliouahidi kwa shule hiyo baada ya kuonekana kuna uhaba wa vifaa vya muziki wa asili shuleni hapo, wanaoshuhudia tukio la makabidhiano hayo katika picha katikati ni walimu Venance Njiku na Bi. Nickyza Bwenge, vifaa hivyo ndivyo vilivyotumiwa na kikundi cha ngoma za asili cha shule hiyo wakati wa mahafali ya shule hiyo yaliyofanyika hivi karibuni shuleni hapo yakishirikisha wazazi, wageni waalikwa mbalimbali , Bodi ya shule pamoja na uongozi wa wanafunzi wa shule hiyo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Pongo Safaris Bi Scholastica Ponera akiwa na Ismail Edward Mkuu wa shule ya Sekondari ya St. Antony Mbagala jijini Dar es salaam wakiwa pamoja na baadhi ya wanafunzi mara baada ya kupokea vifaa hivyo.
4
Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Pongo Safaris Bi. Scholastica Ponera akizungumza na wanafunzi hao mara baada ya kuwatembelea katika mazoezi yao shuleni hapo na kukabidhi vifaa hivyo.
5
Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Pongo Safaris Bi Scholastica Ponera akicheza pamoja na kikundi hicho wakati kikiwa katika mazoezi yake shuleni hapo.
6
Meshack Mahembe mwalimu wa kikundi hicho akifanya mazoezi pamoja na wanafunzi hao.
7
Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Pongo Safaris Bi Scholastica Ponera, Mkuu wa shule hiyo Ismail Edward kulia na na Meshack Mahembe mwalimu wa kikundi hicho wakiwa katika picha ya pamoja.
8
Kikundi cha Ngoma za asili shule ya Sekondari ya St. Antony Mbagala jijini Dar es salaam wakicheza ngoma wakati wa mahafali ya kidato cha Nne yaliyofanyika shuleni hao hivi karibuni.
9
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo akizungumza na wanafunzi na wageni mbalimbali katika mahafali hayo.
10
Mgeni rasmi Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa akiwa katika picha ya pamja na Uongozi wa shule hiyo.

SOURCE FROM MO BLOG

Previous Post Next Post

Popular Items